WATUHUMIWA WATANO WAENDELEA KUSAKWA KWA TUHUMA ZA KUMTEKA MO DEWJI | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, August 20, 2019

WATUHUMIWA WATANO WAENDELEA KUSAKWA KWA TUHUMA ZA KUMTEKA MO DEWJI

  Malunde       Tuesday, August 20, 2019

Upande wa mashtaka katika kesi ya kutekwa kwa mfanyabiashara Mohamed Dewji ‘Mo’ umedai kuendelea na taratibu za kuwatafuta watuhumiwa watano ili kuwaunganishwa katika kesi hiyo.

Hayo yameelezwa leo Jumanne Agosti 20, 2019 na wakili wa Serikali mwandamizi, Wankyo Simon katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Amesema upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na wanaendelea kuwatafuta watuhumiwa hao watano raia wa Msumbiji na Afrika Kusini.

Watuhumiwa hao ni Henrique Simbue, Daniel Berdardo Manchice,Issac Tomu na Zacarious Junior wote raia wa Msumbiji na Phila Tshabalala raia wa Afrika Kusini.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi aliahirisha shauri hilo hadi Septemba 3, 2019.

Mshitakiwa wa kwanza katika kesi hiyo ni Dereva taksi, Mousa Twaleb (46).


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post