MSAFARA WA MAGARI YA KIJESHI WASHAMBULIWA UTURUKI


Shambulio la angani la serikali ya Syria uliolenga msafara wa kijeshi wa Uturuki uliokuwa ukielekea katika eneo linalotawaliwa na waasi kaskazini mwa Syria limesababisha vifo vya raia watatu, Uturuki imedai.

Watu wengine 12 walijeruhiwa katika shambulio hilo katika mkoa wa Idlib siku ya Jumatatu kulingana na wizara ya ulinzi ya Uturuki.

Idlib ambayo ni mojawapo ya maeneo machache yasiodhibitiwa na serikali, ilitarajiwa kulindwa na kuwa eneo huru linalotenganisha majeshi pinzani lililoafikiwa na Uturuki inayowaunga mkono waasi mwaka uliopita.

Lakini mashambulizi ya serikali yamekuwa yakiongezeka tangu mwezi Aprili.

Uturuki inayounga mkono baadhi ya waasi na sio wote ina majeshi yake Idlib kama mojawapo ya makubaliano na Urusi mwaka uliopita.

Kulingana na Naji Mustafa , msemaji wa waasi wa National Liberation Front msafara huo ulikuwa ukielekea katika mojawapo ya vituo vyake vya uchunguzi na walinzi wakati shambulio hilo lilipotokea,

Mwandishi wa AFP ambaye aliuona msafara huo anasema ulishirikisha magari 50 ya kijeshi , matano kati yao yakiwa vifaru.

Lakini Syria imesema kuwasili kwa msafara huo katika eneo hilo ni kitendo cha uchokozi . Imesema kuwa silaha hizo hazitasitisha harakati za wanajeshi wa Syria kukabili kile ilichokitaja kuwa magaidi.

Kulingana na Shirika la haki za kibinadamu la Syrian Observatory for Human Rights (SOHR), lililo na makao yake nchini Uingereza , ndege ya kijeshi ya Urusi ilitekeleza mashambulio karibu na msafara huo tarehe 19 Agosti.

Uturuki imesema kuwa shambulio hilo linakiuka makubaliano ya mwaka uliopita huku kisa hicho kikizua hofu kuhusu makubiliano ya moja kwa moja kati ya mataifa hayo mawili.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527