WATU 10 WANUSURIKA KIFO BAADA YA BOTI KUZAMA TANGA

WATU 10 wamenusurika kifo mmoja akiwa hajulikani alipo baada ya boti waliyopanda kuzama kwenye bahari ya Hindi Jijini Tanga wakati wakiwa wanaenda kuangalia visiwa vilivyopo majini.
Akizungumza leo na Malunde 1 Blog Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Edward Bukombe amethibitisha kutokea kwa tukio Agosti 11,2019 ambapo watu hao walikuwa wamepanda boti waliyokodi kutoka eneo la Yanchi Club.

Amesema baada ya watu hao kupanda boti hiyo walikuwa wakienda kutembelea visiwa mbalimbali vilivyopo kwenye bahari hiyo na ndipo upepo mkali uliwazuia kwenda mbele na walipotaka kugeuza kurudi walipotoka ndipo ilipopinduka na kuwamwaga.

“Watu hao walikuwa wametokea eneo la Yanchi Club walikuwa wanakwenda kutembelea visiwa mbalimbali vya bahari ya Hindi wakati wakiwa njiani upepo mkali uliwazuia kwenda mbele na walipotaka kugeuza kurudi wakapinduka “amesema.

Aidha kamanda Bukombe amesema kwenye boti hiyo iliyokuwa na watu 11 ambapo 10 kati yao waliweza kuokolewa kutokana na kuvaa maboya wakati wakiwa baharini na mwengine mmoja ambaye inadaiwa hakuwa nayo mpaka sasa hajulikani alipo.
“Nitoa wito kwa wananchi wanaotumia bahari kusafiria kuchukua
tahadhari wanapokuwa bahari kwa kuhakikisha wanavaa maboya ya kujiokolea ili wakati yanapotokea majanga kama hayo waweze kuona namna ya kujiokoa “amesema Kamanda huyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post