WADAU WAKUTANA DODOMA KUJADILI USAWA WA KIJINSIA KUFIKIA 50% KWA 50% KWENYE UONGOZI


Serikali imesema imeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa wanawake wanashirikishwa katika nafasi mbalimbali za uongozi ya 50 kwa 50 kufikia mwaka 2025.


Mkakati huo ni kufuatia serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuridhia kutekeleza malengo endelevu ya dunia likiwemo lengo namba 5 linalohusu usawa wa kijinsia ifikapo mwaka 2030.

Akizungumza katika kongamano la kuwaleta pamoja wadau katika kuzungumzia usawa wa kijinsia hasa katika kuwashirikisha wanawake na wasichana katika ngazi mbalimbali za uongozi na maamuzi,lililofanyika leo jijini Dodoma, mkuu wa mkoa wa Dodoma Dk. Benelith Mahenge amesema kongamano limedhihirisha wananchi wanakusudia kufikia mikakati ya 2025 na malengo endelevu ya 2030.

Awali mbunge wa viti maalum Mkoa wa Dodoma Fatma Taufiq ambaye pia ni Mwenyekiti wa shirika la Achieve SDG5 Coalition in Tanzania,amesema lengo la kongamano hilo ni kuhakikisha vikwazo vinavyowakumba wanawake kushindwa kufikia lengo namba 5 katika malengo endelevu ya dunia vinapatiwa ufumbuzi.

Amesema kuwa kutokana na kuwa wafanyakazi wa ndani ni wanawake wanapata stahiki zao za malipo sambamba na ushiriki wao wa kupata nafasi za uongozi na kutoa maamuzi.

Hata hivyo baadhi ya washiriki wa kongamano hilo wamesema moja ya vikwazo violivyokuwa vinawakumba wanawake ni pamoja na rushwa katika maeneo ya kazi.

Kongamano hilo limeambatana na ujumbe usemao “Lengo namba tano la malengo endelevu litafikiwa kwa kuwawezesha wanawake na wasichana kushiriki kikamilifu katika ngazi zote za uongozi na maamuzi, Kufikia asilimia 50 % kwa 50% inawezekana.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527