UTURUKI YAPANGA KUNUNUA NDEGE YA KIVITA ILIYOTENGENEZWA URUSI CHAPA SU-57 | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, August 28, 2019

UTURUKI YAPANGA KUNUNUA NDEGE YA KIVITA ILIYOTENGENEZWA URUSI CHAPA SU-57

  Malunde       Wednesday, August 28, 2019

Viongozi wa Urusi wanazungumza na wenzao wa Uturuki kuhusu uwezekano wa kuiuzia Ankara ambayo ni mwanachama wa jumuia ya kujihami ya NATO ndege za kivita chapa Su-57. Afisa mmoja wa ngazi ya juu wa Urusi amesema.

Rais Recep Tayyip Erdogan ameonyeshwa ndege hiyo ya ufundi wa kimambo alipohudhuria maonyesho ya ndege za kivita mjini Moscow.

Ndege hiyo inalinganishwa na ile ya kivita ya Marekani chapa F-35. 

Marekani ambayo pia ni mwanachama wa NATO imeamua hivi karibuni kuitoa Uturuki katika mradi wake wa ndege ya kivita chapa F-35, baada ya Uturuki kununua kutoka Urusi mtambo wa kinga ya angani dhidi ya makombora, S-400.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post