UTEKELEZAJI WA KATAZO LA MIFUKO YA PLASTIKI WAPOKELEWA VIZURI NA WANANCHI

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima amesema utekelezaji wa Marufuku ya matumizi ya mifuko ya plastiki nchini umepokelewa na wananchi kwa mtazamo chanya na Serikali inaendelea kuratibu usimamizi wa katazo la Mifuko ya plastiki kikamilifu kwa kuweka usimamizi madhubuti wa matumizi ya mifuko mbadala.

 
Akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa agizo la kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya Plastiki; mwitikio wa jamii kuhusu katazo la kutumia mifuko ya plastiki na mipango ya serikali katika kuhakikisha upatikanaji wa mifuko mbadala ambayo ni imara na kwa bei mbele ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. Sima amewahihikishia wajumbe wa Kamati hiyo kuwa agizo linaendelea kusimamiwa na Serikali kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na taratibu zilizopo. 

Kwa upande wao baadhi ya Wajumbe wa Kamati hiyo wametoa pongezi kwa Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kuratibu utekelezaji wa katazo hilo la mifuko ya plastiki hapa nchini.

Aidha wajumbe hao walipendekeza sheria iwabane zaidi wazalishaji wa mifuko iliyokatazwa pamoja na wafanyabiashara wanaowafungia bidhaa watumiaji wa mwisho.

Pamoja na kutoa pongezi pia walizungumzia ubora wa baadhi ya mifuko mbadala ya 'non woven' wakisema kuwa haiwezi kuhimili bidhaa zenye uzito mkubwa.

Kutokana na changamoto hiyo waliiomba Serikali kutoa maelekezo kwa wazalishaji wa mifuko hiyo kuzalisha yenye ubora unaotakiwa ambayo haichaniki kwa urahisi ili wananchi waweze kuitumia.

Mjumbe huyo pia aliiomba Serikali kushughulikia tatizo la kupaa kwa bei ya mifuko mbadalana kusema kuwa mwananchi analazimika kununua mifuko badala ya kununua bidhaa aliyokusudia.

Kwa upande mwingine wajumbe walitoa mwito kwa Serikali kuimarisha ulinzi katika mipaka ya nchi wakisema kuwa mifuko mingi ya plastiki imekuwa ikipita mipakani na kuingia nchini.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post