TIGO YAZINDUA MNARA WA 3G KISAKI MKOANI MOROGORO


Meneja Mauzo wa Tigo mkoa wa Morogoro Frank Antony, akiongea na wakazi wa mji wa Kisaki baada ya hafla ya uzinduzi wa mnara wa Tigo wa 3G (kulia) ni Mwenyekiti wa kijiji cha Gomero, Shime Hassan Shime.

Afisa mtendaji wa kata ya Kisaki, Shaibu Nampesya, (wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Tigo baada ya kuzindua mnara wa mawasiliano wa 3G katika kata hiyo mwenye shati jeupe ni Meneja Mauzo wa Tigo mkoa wa Morogoro, Frank Antony

Kampuni inayoongoza kwa kutoa huduma za mawasiliano ya Tigo Tanzania, imezindua mnara wa intaneti ya 3G katika eneo la Kisaki Morogoro.

Akiongea wakati wa uzinduzi, Meneja Mauzo wa Tigo mkoani Morogoro, Frank Antony, alisema upatikanaji wa huduma hiyo ya 3G katika eneo hilo utafanikisha kuboresha huduma za kijamii sambamba na kukuza shughuli za uchumi .

“Kuzinduliwa kwa mnara wa 3G hapa Kisaki, kunawezesha wateja wetu kutumia na kufurahia ubunifu wa huduma zetu za kidigitali sambamba na kupata maudhui ya kuelimisha, kuburudisha, kupata taarifa za biashara, sambamba na kuleta mabadiliko chanya katika shughuli za ukuzaji uchumi. Pia watapata intaneti yenye kasi kubwa na mawasiliano bora ya huduma ya maongezi kupitia simu zao za mkononi” alisema Antony.

Aliongeza kusema kuwa “Uzinduzi huu unaenda sambamba na kuwapatia ofa wateja wa Tigo watakaojiunga na kifurushi chochote cha data kupatiwa MB100 kila siku kwa muda wa siku 30. Ofa hii itadumu kwa muda wa siku 30 tangu siku ya uzinduzi wa mnara”.

Uzinduzi huu ni mwendelezo wa kampuni kuzindua minara ya kuboresha mawasiliano ambapo tayari umefanyika sehemu mbalimbali nchini. Mnara huu ni wa 10 kati ya minara 52 ambayo mawasiliano yake yataboreshwa kuwa ya 3G na 4G LTE, katika mikoa ya Kati, Pwani, Kusini, Kaskazini na Kanda ya Ziwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post