'ZOEZI KIKAKA' YAAHIRISHWA.....WANAJESHI WAJIIMARISHA KULINDA MAPORI KIGOMA

Na Rhoda Ezekiel -Malunde1 blog  Kigoma
Mkuu wa Brigedi ya Magharibi 202 KV,Brigedia jenerali Jackobo Mkunda amewataka Wanajeshi wa Kikosi cha 24 Kj, kuhakikisha wanaendelea kukaa na kukagua ulinzi na usalama katika ofisi zao ambazo ni Mapori ya Mkoa wa Kigoma ili kuhakikisha mpaka wa magharibi unakuwa salama na hauvamiwi na watu waovu.

Wito huo aliutoa jana wakati wa akiahirisha Mafunzo ya siku 13 yaliyofahamika kama 'Zoezi Kikaka', yaliyohusisha kombania kujifunza namna ya kukabiliana na maadui, kuainisha matumizi ya silaha za kivita ,kutathimini utendaji kazi wa silaha za kikosi,kuimarisha utendaji kazi wa kikosi, kuwezesha maafisa kujua matumizi ya silaha za kivita katika nyakati zote na kuwajengea uwezo maafisa wa kutoa amri na matumizi ya redio nyakati za vita.

Alisema zoezi hilo litakuwa endelevu na hawatakubali kuona misitu na mapori yanavamiwa na raia kutoka nje ya nchi, wanaotumia mapori hayo kufanya uharifu na kuwatishia usalama wananchi wa Mkoa wa Kigoma, jeshi litahakikisha linalinda amani na usalama wa maeneo hayo kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama.

Brigedia Mkunda alisema ili kuhakikisha Wanamuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli katika adhima yake ya uchumi wa viwanda ni lazima wahakikishe nchi iko salama na wananchi wanafanya shughuli zao bila kuwa na bugha yoyote na kuhakikisha amani inaendelea kuwepo.

"Kazi ya kuhakikisha ofisi zao ziko salama ni haki yao askari wa Jeshi la Wananchi hivyo kuzijua ofisi zao na wanapaswa kuzilinda na kuhakikisha muda wote ziko salama , kwa kipindi chote cha mafunzo wameweza kujiimarisha vizuri zaidi na zoezi hilo ni endelevu nipende kuwahakikishi Wwananchi kuwa eneo hilo ni salama na wafanye kazi kwa uhuru', alisema brigedia Mkunda.

Alisema suala la ulinzi na usalama sio la Jeshi pekee, bali kila taasisi pamoja na wananchi wanatakiwa kuwafichua Watu wote wanaoingia nchini bila vibali na kufanya uharifu pamoja na raia wanaoshirikiana nao katika vitendo hivyo.

Naye Mkuu wa mafunzo na utendaji kivita kikosi 202KV Kanali Wilson Ibuge alieleza kuwa mapori yanapoonekana hayana watu yana mwenyewe na mwenyewe ndiyo Jeshi la Wananchi na zoezi ndiyo kwanza limeanza, kazi ya jeshi ni vita hawapendi vita na iliwaweze kutekeleza vita lazima wajiandae na sehemu pekee ni mafunzo ya kivita na mazoezi.

Alisema matarajio ya brigedi siyo tu eneo la miliki ya kikosi cha 24 kj zoezi hilo ni endelevu na linapeleka salamu kwa wavamizi wa maeneo hayo na wakitaka salama ni kuacha kujihusisha na mambo ya kijangili na uharifu na pamoja na Wananchi wa Tanzania wanaoshirikiana na Warundi kufanya uharifu wote watashughulikiwa ipasavyo.

Aidha kamanda wa kikosi cha 24 KJ Meja Jonson Luhovyq alisema kuwa ndani ya siku kumi na tatu za mafunzo hayo askari wameweza kufanya zoezi hilo katika maeneo ya Malagarasi, Mvugwe, Kagerankanda, Busunzu,Nyarugusu na Kisogo pamoja na maeneo yanayo karibia kambi ya Kanembwa.

Alisema katika zoezi hilo waliweza kubaini baadhi ya raia kutoka nchi jirani ya Burundi, kuwepo katika eneo la mapori hayo wanaojihusisha na uvunaji wa mihogo baada ya hapo wanajihusisha na mambo mengine ya kihalifu.

Alisema watahakikisha wanalinda maeneo hayo pamoja na askari kufanya mafunzo hayo wataweza kushirikiana na Jeshi la polisi kulinda amani ha maeneo ya mpakani, na katika zoezi hilo matokeo makubwa yamepatikana na litakuwa endelevu.

Hata hivyo alisema changamoto waliyonayo ni ukosefu wa mafuta, endapo wakipata lita 300 kila mwezi, wataweza kuendelea na mazoezi hayo katika mapori ilikuhakikisha maeneo hayo yanakuwa salama na hakuna uharifu.

Kwa upande wake, mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Simon Hanange aliwapongeza askari kwa kazi kubwa walioifanya, na kuswma kwamba poti hilo lazima lilindwe kwa kuwa eneo kubwa la pori hilo ni chanzo cha mto Maragalasi linalomwaga maji katika Ziwa Tanganyika endapo litahaeibiwa litasababisha kuongezeka kwa joto ziwani na kusababisha madhara pamoja na samaki kukimbia.

Alisema serikali ina mpango wa kuboresha bandari ya mkoa wa Kigoma ni lazima zipwa liendelee kulindwa na kuwa la kisasa kwa kuwa bandari inategemea ziwa kazima msitu huo ulindwe, serikali itaendelea kushirikiaka na jeshi kuhakikisha katika mapori hayo hakuna kilimo kinachofanyika wala kuwepo na vitendo vya uharifu.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527