TANZANIA YASEMA IKO TAYARI KUWAPOKEA WAKUU WA NCHI NA SERIKALI KWA AJILI YA MKUTANO WA 39 WA SADC

Serikali imesema maandalizi ya shughuli za SADC yamekamilika kwa kiwango kikubwa na sasa Tanzania iko tayari kuanza kupokea wageni na viongozi waandamizi wa Nchi 16 wanaotarajiwa kuhudhuria mkutano wa SADC unaofanyika Dar es Salaam Tanzania.Akizungumza wakati wa ukaguzi wa magari yatakayotumiwa na viongozi mbalimbali watakaohudhuria mkutano huo wa SADC Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi amesema,maandalizi yamekamilika baada ya shughuli ya ukaguzi na kujiridhisha kuhusu utayari wa kuwapokea wageni.

Ameongeza kuwa Serikali imejiridhisha kuwa ina uwezo na iko tayari kuwapokea wageni na viongozi wakiwemo marais wa Nchi 16 za ukanda wa kusini mwa Afrika baada ya kukagua mahali watakapofikia,sehemu ya kufanyika kwa mikutano mbalimbali na mambo mengine muhimu kwa wageni hao.

Aidha, Prof. Palamagamba John Kabudi ameeleza kwa uchache utaratibu wa viongozi wakuu wa Nchi na Serikali watakavyoanza kuwasili kwa kufafanua kuwa marais na wafalme wanatarajiwa kuanza kuwasili Agust 16,2019, licha ya ukweli kuwa shughuli za SADC zimekwishaanza toka August 05,2019 ambayo ilikuwa na wiki ya maonesho ya viwanda na jana ilikuwa ni siku ya kilele ambapo Mgeni rasmi wa kufunga maonesho hayo ya viwanda alikuwa ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Mohamed Shein


Bw. Zuberi Kachingwe Afisa Usafirisahaji, IKULU,(katikati) akitoa maelezo kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akikagua magari yatakayotumiwa na viongozi na Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kujiridhisha juu ya matayarisho ya mapokezi kwa ajili ya mkutano huo utakaofanyika Dar es Salaam,Tanzania. Kulia ni Afisa Usafirishaji Msaidizi Bw. Athumani Natepe. August 8, 2019.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Bw. Zuberi Kachingwe Afisa Usafirisahaji, IKULU pamoja na Bw. Athumani Natepe Afisa Usafirishaji Msaidizi mara baada ya kumaliza kukagua magari yatakayotumiwa na viongozi na Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) mkutano utakaofanyika Dar es Salaam,Tanzania. August 8, 2019.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa amesimama mbele ya magari yanayotarajiwa kutumiwa na viongozi na Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kujiridhisha juu ya matayarisho ya mapokezi kwa ajili ya mkutano huo utakaofanyika Dar es Salaam,Tanzania. August 8, 2019.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa ndani ya mojawapo ya magari yanayotarajiwa kutumiwa na viongozi na Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kujiridhisha juu ya matayarisho ya mapokezi kwa ajili ya mkutano huo utakaofanyika Dar es Salaam,Tanzania. August 8, 2019.


Baadhi ya magari yanayotarajiwa kutumiwa na viongozi,wakuu wa Nchi na Serikali wakati wa mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) mkutano utafanyika Dar es Salaam,Tanzania. August 8, 2019.


Baadhi ya magari yanayotarajiwa kutumiwa na viongozi,wakuu wa Nchi na Serikali wakati wa Mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) mkutano utafanyika Dar es Salaam,Tanzania. August 8, 2019.Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post