TETESI ZA SOKA LEO JUMANNE AGOSTI 27,2019

Huenda Manchester United ikasubiri ukaguzi wa mchezaji wa kiungo cha mbele raia wa Ufaransa Anthony Martial, mwenye umri wa miaka 23, kabla ya kuruhusu uhamisho wa mkopo wa mchezaji wa kimataifa wa Chile Alexis Sanchez, mwenye umri wa miaka 30, kwenda Inter Milan. (Guardian)

Paris St-Germain imeambia Real Madrid itatafakari kumuuza mchezaji wa Brazil wa kiungo cha mbele Neymar, mwenye umri wa miaka 27, iwapo mchezaji wa klabu hiyo ya Uhispania mwenye miaka 19 na mshambuliaji wa Brazil Vinicius Jr iatakuwa sehemu ya makubaliano ya kudumu. (AS)

Wakurugenzi wa Barcelona wamekutana Jumatatu kujadili ombi la mchezaji wao wa zamani Neymar. (Marca)

Huenda Inter Milan ikamgeukia mchezaji wa kiungo cha mbele wa Manchester City Wilfried Bony, mchezaji huyo wa Ivory Coast mwenye miaka 30 kwa sasa haichezei klabu yoyote baada ya kuachiwa na Swansea msimu wa joto. (Goal.com)

Mchezaji wa kimataifa wa Serbia Nemanja Matic, mwenye umri wa miaka 31, ameitisha mazungumzo na meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer baada ya kuipoteza nafasi yake ya kwanza huko Old Trafford. (Mirror)

Arsenal ipo tayari kumruhusu mchezaji wa kimataifa wa Uhispani Nacho Monreal kujiunga na Real Sociedad wiki hii iwapo mchezaji huyo wa miaka 33 na mchezaji wa kiungo cha ulinzi ataomba kuondoka. (Sun)

Javi Gracia anapigania kuokoa nafasi yake kama meneja wa Watford baada ya kuanza msimu wa ligi kuu England kwa kushindwa mara tatu. (Telegraph)
Mshambuliaji wa Chelsea Tammy Abraham anaelekea kupata mkataba mpya ambao huenda ukaongeza zaidi ya mara mbili malipo ya mchezaji huyo wa miaka 21 raia wa England ya £50,000 kwa wiki(Telegraph)

Wawakilishi wa Christian Eriksen hawatofikiria pendekezo la mkataba wa Tottenham la malipo ya £200,000 kwa wiki na mchezaji huyo wa miaka 27 ambaye mkataba wake hivi sasa unamalizika msimu ujao wa joto anatumai kupata uhamisho kwenda Uhispania. (Mirror)

Eriksen ni kama amejiuzulu kusalia Tottenham katika kipindi kifupii, huku ndoto yake ya kujiunga na Real Madrid au Barcelona msimu huu wa joto ikishindwa kufanikiwa. (Mail)

Winga wa Celta Vigo Pione Sisto, mwenye umri wa miaka 24, anakaribia kujiunga na Torino baada ya uhamisho kwenda Aston Villa kutofanikiwa. (Marca)

Mabingwa wa Italia Sampdoria wanataka kumsajili winga wa Swansea anayeichezea timu ya taifa ya Ghana Andre Ayew, mwenye umri wa miaka 29, kwa mkopo kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho Ulaya (Star)
Mlinzi wa Manchester United Luke Shaw, mwenye miaka 24, huenda akawa nje kwa hadi mwezi mmoja kutokana na jeraha katika msuli wake wa paja. (Talksport)

Huenda Sunderland ikawasilisha ombi la pili kwa mlinzi wa Sheffield Morgan Fox, 25 hapo kesho Jumatano (Newcastle Chronicle)

Jurgen Klopp anaamini mbinu yake ya usimamizi inaongeza uwezekano wa yeye kwenda mapumzikoni wakati kipindi chake cha usimamizi kitakapomalizika Liverpool mwaka 2022. (Times)

Kevin De Bruyne ameunga mkono mchezaji wa zamani wa timu ya Manchester City , Vincent Kompany kuwanyamazisha wakosoaji na kufungua ufanisi wa nafasi yake mpya kama bosi wa Anderlecht, baada ya kujizolea pointimbili katika mechi nne za kwanza msimu huu. (Manchester Evening News)

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Spurs na timu ya taifa ya Kenya Victor Wanyama amepewa mkataba wa miaka mitano kwa malipo ya £65,000- kwa wiki na Club Bruges wakati anapokaribia kukamilisha uhamisho. (Scottish Sun)Mchezaji wa kiungo cha kati wa Spurs na timu ya taifa ya Kenya Victor Wanyama

Kalbu ya Fiorentina katika ligi ya Serie A inajitayarisha kuwasilisha ombi kwa mchezaji wa kiungo cha kati wa Manchester United na timu ya taifa ya Brazil Fred, mwenye umri wa miaka 26. (Calciomercato)

Norwich itamfukuzia kipa wa Stoke na timu ya taifa ya England Jack Butland, mwenye umri wa miaka 26, ifikapo Januari na iwapo thamani yake itashuka. (Sun)

Bordeaux inataka kumchukua mchezaji wa kiungo cha kati wa Arsenal na Misri Mohamed Elneny, mwenye umri wa miaka 27, kwenda Ligue 1 kwa mkopo. (Foot Mercato)

Leeds inatarajiwa kuanza mara moja mazungumzo na mchezaji wa kiungo cha kati Kalvin Phillips kuhusu mkataba mpya. Mchezaji huyo wa miaka 23 anataka kulipwa £40,000 kwa wiki ili kuendelea kusalia Elland Road. (Football Insider)

Aliyekuwa beki kamili wa Chelsea Filipe Luis, mwenye umri wa miaka 34, amekataa ombi la Manchester City, Lyon na Borussia Dortmund msimu huu wa joto kabla ya kujiunga na Flamengo kutoka nchini anakotoka Brazil. (Globo Esporte)Beki kamili wa zamani wa Chelsea Filipe Luis

Aliyekuwa beki wa kulia wa Leicester Danny Simpson, mwenye umri wa miaka 32, anafanya mazungumzo na klabu ya Ligue 1 - Amiens kuhusu uhamisho. (Sun)

Meneja wa Chelsea Frank Lampard amemkaribisha mchezaji wa kiungo cha kati wa Exeter Ben Chrisene kufanya mazoezi na klabu hiyo. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 15 kutoka timu ya vijana wa timu ya taifa England alifanikiwa kucheza katika kikosi cha kwanza mwezi huu. (Sun)
Chanzo - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post