ANUSURIKA KIFO BAADA YA KICHWA CHAKE KUKWAMA KWENYE NGAZI SIKU 5


Hili halikuwa katika muogozo wa ukarabati: mwanamume aliyekuwa anajaribu kukarabati na kulirembesha bafu lake huko mashariki mwa Ufaransa aliteleza akaanguka na kukwamisha kichwa chake kwenye ngazi kwa siku tano.

Vyombo vya habari nchini humo vinaeleza kuwa, mwanaume aliye katika miaka ya 60 alikuwa amepotewa na fahamu wakati wahudumu wa afya walipowasili.

Waliarifiwa na dadake , aliyemtembelea siku ya Ijumaa.

Kichwa chake , kilichokwama katikati ya ngazi , kilifura katika siku hizo tano na alishindwa kuifikia simu yake kuomba usaidizi.

Msukumo wa damu kichwani mwake ulipungua, na anafanyiwa ukaguzi hospitalini.

Jamaa huyo anayetoka Mattaincourt karibu na Épinal, ambaye jina lake halikuwekwa wazi alipatikana akiwa hana maji mwilini.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post