KIMBUNGA KAGERE CHAIHARIBU VIBAYA POWER DYNAMOS


Na Olipa Assa Charity James 
 Mshambuliaji Meddie Kagere ameipamba Simba Day kwa kufunga mabao matatu peke yake akiongoza Simba kuichapa Power Dynamos 3-1 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Katika mchezo huo wa kirafiki Kagere mfungaji bora wa msimu uliopita alifunga mabao yake katika dakika 3, 58 na 73, na kuacha shangwe kubwa kwa mashabiki 60,000 wa Simba waliojitokeza uwanjani hapo.


Kagere aliyezoeleka kwa mtindo wake wa kufunga jicho moja, lakini leo aliingia kwa mtindo tofauti wa kushangilia kuinama kidogo huku akiwa amenyosha mkono kama anapaa alipofunga bao la kwanza.

Katika bao la pili Kagere alipiga goti na kusujudu kabla ya lile la tatu alilokwenda kwa mchukua video na kujipa kazi hiyo jambo lililowalipua mashabiki wa Simba kwa shangwe.

Katika mchezo huo wachezaji wapya wa Simba walikonga nyoyo za mashabiki wa Simba,a kiungo Msudani Sharaf Eldin Shiboub pamoja na Mkenya Francis Kahata kutokana na uwezo wako wa kutawala mchezo.

Shiboub ananyumbulika licha kucheza kiungo mkabaji, lakini amekuwa akiibia kupeleka mipira mbel

Msudani huyo amevaa jezi namba nane ambayo aliitumia Haruna Niyonzima ambaye waliachana naye baada ya kutokuwa na msimu mzuri.

Wabrazili beki Tairone, na kiungo Gerson Vieira wamethibisha wamekuja Tanzania kufanya kazi baada ya kucheza kwa kiwango cha juu katika mchezo huo na kumaliza utata wa uwezo wao.

Katika mchezo huo Simba ilianza kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la mapema dakika tatu baada ya kipa Dynamos, Lawrence Mulenga kushindwa kuokoa pasi aliyorudishwa.

Dynamos ilijibu mapigo kwa kupata bao la kusawazisha kupitia kwa Jimmy Dlingai aliyeunganisha kwa kichwa mpira wa kona uliopigwa na Konchwani Chibori katika dakika ya 24.

Kipindi cha pili timu zote zimeanza kwa kusoma mchezo na kushambuliana kwa zamu.

Kila upande ulionekana kuhitaji bao la kuongoza dakika ya 48 Simba walifanya mabadiliko kwa kumtoa Shiboub kuiingia Gerson Vieira.

Mabadiliko hayo yalikuwa na faida kwao kwani dakika ya 58, Deo Kanda alipiga krosi iliyomkuta Kagere na kukwamisha mpira nyavuni kwa kichwa.

Kagere baada ya kufunga bao la pili kwa kichwa mashabiki wa Simba waliwasha taa za simu zao, huku uwanja ukilindima shangwe za aina yake.

Siyo kwamba umeme umekatika taa walizowasha mashabiki hao ni kama ishara ya kuonyesha furaha yao kwa kile kinachofanywa na mastaa wao.

Kagere amepigilia msumali wa tatu dakika ya 73 akipokea pasi safi kutoka kwa Chama.


Dakika ya 74 Simba wamefanya mabadiliko kwa kumtoa Kanda na nafasi yake kuchukuliwa na Rashid Juma.

Simba iliendelea kutawala mchezo huo hadi dakika 90 zinamalizika na kuwafanya mabingwa hao kufungua msimu wao kwa kishindo.

Ushindi huo unaiweka Simba katika nafasi nzuri wakati wakijiandaa na safari ya kwenda Msumbiji kuivaa UD Songo katika mchezo awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kikosi cha Simba

Kakolanya, Kapombe, Tshabalala, Tairone, Wawa, Mzamiru, Kanda, Shiboub, Kagere, Chama Kahata

Akiba: Ally Salum, Yusuph Mlipili, Kennedy Juma, Said Ndemla, Tairone Gerson Vieira, Rashid Juma, Miraji Athuman

Power Dynamos: Lawrence Mulenga, Larry Bwalya 8, Raphael Makubali 35, Jimmy Dlingai 20, John Soko 15, White Mwambaba 27, Benson Sakala 6, Konchwani Chibori 4, Christian Ntiba 21, Fredrick Mulamba 26, Kasim Titus 19
Chanzo - Mwanaspoti

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post