RAIS WA ZANZIBAR DK SHEIN ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI AJALI YA LORI LA MAFUTA MOROGORO


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk. Kebwe Stephan Kebwe, kufuatia ajali ya kuripuka kwa lori la mafuta na kusababisha vifo pamoja na majeruhi kadhaa. 


Amesema yeye binafsi pamoja na wananchi wote wa Zanzibar anatuma salamu za rambirambi kwa wanafamilia wa marehemu, marafiki, wananchi wa Mkoa wa Morogoro na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jumla.

Katika salamu hizo  Rais Shein alimuomba mwenyezi Mungu awalaze mahala pema wote na awape nafuu ya haraka majeruhi wa ajali hiyo ili waweze kupata shifaa na waendelee na majukumu yao mbalimbali ya ujenzi wa Taifa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post