JESHI LA POLISI LATAJA IDADI KAMILI YA MAREHEMU NA MAJERUHI WA AJALI YA MOTO MKOANI MOROGORO

Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo Lebaratus Sabas,  ameitaja idadi ya watu waliofariki katika ajali ya gari iliyoanguka nakupelekea kulipuka kwa moto leo Agosti 10,  imefikia 62.

Ameeleza kuwa kati yao wanaume ni  58 na wanne ni wanawake ambapo mmoja katika wanawake hao ni mtoto.

Kwa upande wa idadi ya majeruhi imefikia  72, wanawake wakiwa 8 na wanaume 64 ambapo wote wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hosptali ya rufaa ya Morogoro.

Ajali hiyo imetokea majira ya asubuhi katika eneo la Msamvu Mkoani Morogoro na hadi sasa Jeshi la polisi,  limekwishakamata lita takribani 206 za mafuta ya petroli , zilizokuwa zimefichwa katika mabanda pembezoni mwa eneo la ajali ilipotokea.

''Pia katika eneo la  tukio zimepatikana pikipiki zilizoungua kwa moto zipatazo 26 na baiskeli 6, pia yamaeonekana mabaki ya madumu na ndoo za plastiki zilizoungua'' amesema Kamishna Sabas.

Aidha Kamishina Sabas amewataka wananchi wanaoishi kandokando  ya barabara kutokuwa na tamaa na kujiepusha na ajali ambazo zinaepukika, pamoja na kuwataka wale wote waliopata majeraha madogomadogo na  kutokomea wasisite kwenda hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527