RAIS WA ZAMAN WA SUDAN MAHAKAMANI TENA LEO....AMEKIRI KUPEWA DOLA MILIONI 90 NA SAUDI ARABIA | MALUNDE 1 BLOG

Monday, August 19, 2019

RAIS WA ZAMAN WA SUDAN MAHAKAMANI TENA LEO....AMEKIRI KUPEWA DOLA MILIONI 90 NA SAUDI ARABIA

  Malunde       Monday, August 19, 2019

Upande wa mashitaka katika kesi ya ufisadi inayomkabili rais wa zamani wa Sudan, Omar al-Bashir, umeiambia mahakama mjini Khartoum leo kuwa kiongozi huyo amekiri kupokea dola milioni 90 taslimu kutoka kwa Ufalme wa Saudia Arabia.

Brigadia Ahmed Ali alisema Bashir alimuambia kuwa malipo ya mwisho yaliwasilishwa kwake na baadhi ya wajumbe wa mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudia, Mohammed bin Salman. 

Afisa huyo wa upelelezi aliiambia mahakama kuwa walikuta kiasi cha euro milioni saba pamoja na kiwango kidogo cha dola za Kimarekani na paundi za Sudan kwenye makaazi ya Bashir, ambaye alisema zilikuwa sehemu ya kitita cha dola milioni 25 ambazo Bin Salman alimpa kwa matumizi yaliyo nje ya bajeti. 

Bashir alisema alikuwa amepokea malipo mara mbili ya dola milioni 35 na milioni 30 kutoka kwa Mfalme Abdullah wa Saudi Arabia aliyefariki dunia mwaka 2015. 

Bashir ambaye aliitawala Sudan kwa miaka 30, alifikishwa mahakamani leo akisindikizwa na msafara mkubwa wa kijeshi.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post