RAIS MAGUFULI AIOMBA JUMUIYA YA KIMATAFA KUIFUTIA VIKWAZO VYA KIUCHUMI ZIMBABWE

Rais  Magufuli ameiomba Jumuiya ya Kimataifa kuiondolea vikwazo vya kiuchumi nchi ya Zimbabwe ambapo amesema kuwa vikwazo hivyo vimelemaza uchumi wa taifa hilo.


Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Agosti 17, alipokuwa akihutubia wakuu wa nchi Wanachama Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), baada ya kukabidhiwa uenyekiti wa jumuiya hiyo na Rais wa Namibia, Dk Hage Geingob ambapo ataingoza kwa kipindi cha mwaka mmoja.

"Zimbabwe wamekuwa kwenye vikwazo kwa muda mrefu, hiki kifungo tunaathirika sisi wote, napenda kupendekeza kupitia mkutano huu kuziomba Jumuiya za Kimataifa ziiondolee vikwazo Zimbabwe, na nawaomba wanachama wote tulisemee hili." amesema Rais Magufuli

Zimbabwe iliwekewa vikwazo na mataifa ya Magharibi kutokana na hatua ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Robert Mugabe, kuchukua kwa lazima ardhi ya wahamiaji wenye asili ya kizungu.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post