NDEGE YAANGUKA NA KUTEKETEA MOTO IKITOKEA MAFIA KWENDA DAR


Kamanda wa Polisi kanda Maalumu ya Rufiji Onesmo Lyanga, amethibitisha kutokea kwa ajali ya ndege ndogo ya shirika la Tropical, iliyokuwa ikiruka kutoka katika kiwanja cha ndege cha Mafia kuelekea Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi kanda Maalumu ya Rufiji Onesmo Lyanga.

Kamanda Lyanga amesema ajali hiyo imetokea leo Agosti 6,2019 majira ya saa 4:00 asubuhi, baada kuanguka na kuteketea kwa moto na ilikuwa na abiria takribani tisa.

''Ndege imepata ajali ilikuwa inaruka uwanja wa Mafia kwenda uwanja wa Julius Nyerere Dar es salaam, ilikuwa na watu 9 lakini mpaka sasa hivi hakuna aliyefariki na kuna majeruhi 6 na ndege yote imeteketea.

Aidha kamanda amesema kuwa majeruhi wote 6 wamekimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu zaidi na kwamba Jeshi la polisi Mkoani humo linaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha ajali hiyo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527