Makubwa Haya : MWANAMICHEZO MWANAUME AKUTWA NA UJAUZITO | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, August 6, 2019

Makubwa Haya : MWANAMICHEZO MWANAUME AKUTWA NA UJAUZITO

  Malunde       Tuesday, August 6, 2019

Mwanamichezo wa mpira wa kikapu nchini Marekani Donell Cooper
Mwanamichezo wa mpira wa kikapu nchini Marekani Donell Cooper, amezua gumzo ulimwenguni baada ya kupimwa mkojo na kukutwa mjamzito wakati anafanya vipimo vya afya ili kujiunga na timu nchini Bosnia Herzogovina.

Inadaiwa kuwa mchezaji huyo ametumia mkojo wa mpenzi wake ili kukwepa kupimwa kwa sababu alikuwa anatumiwa dawa za kuongeza nguvu.

Kipimo cha kumgundua mtu anayetumia madawa ya kulevya kiitwacho Human Chorionic Gonadotropin (HGO) kimeonyesha kuwa mchezaji huyo ni mjamzito.

Baada ya kugundulika kuwa ametumia mkojo wa mpenzi wake Donell Cooper amesema hata yeye alikuwa hajui kama mpenzi wake ni mjamzito na amefanya hivyo ili kukwepa kugundulika kama anatumia dawa ya kuongeza nguvu.

Mchezaji huyo wa zamani wa timu ya Monaco na Ohio kwa sasa amefungiwa miaka 2 na chama cha mpira wa kikapu duniani (FIBA) kutojiuhusisha na mchezo huo.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post