NAIBU WAZIRI WA MALIASILI AAGIZA WANANCHI WALIOVAMIA MSITU WA HIFADHI GAIRO WAKAMATWE

FARIDA SAIDY, MOROGORO

Naibu waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe.Constantine Kanyasu ameagiza kukamatwa kwa  wananchi wote waliovamia na kukata miti bila kufuata taratibu za kisheria katika msitu wa hifadhi ya kijiji cha Kumbulu uliopo wilaya ya Gairo mkoani Morogoro.

Naibu waziri ameyasema hayo alipotembelea eneo hilo na kujionea uharibufu mkubwa uliofanywa na baadhi ya wananchi waliovamia msitu huo licha ya kufahamu eneo hilo lilitengwa kuwa hifadhi ya serikali ya kijiji tangu mwaka 2008 akilenga kutafuta ufumbuzi wa mgogoro baina ya serikali ya kijiji na wananchi.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Gairo Bi. Siriel Nchemba amesema mgogoro huo umedumu kwa muda mrefu na hatua za ufumbuzi kwa ngazi ya wilaya zilielekea kushindikana, kutokana na vitisho kutoka kwa viongozi wa juu serikalini ambapo tayari baadhi ya viongozi wameondolewa katika nafasi zao.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527