WANANCHI WAPEWA DAWA YA KUKOMESHA MIRADI HEWA YA MAENDELEO



Kulia ni  Mratibu wa shirika la Faraja For Hope And Development Organisation ,Shakira Omary  akiwa na Mwezeshaji kutoka katika shirika hilo Andochius Kamuhabwa.  

Na Lydia Lugakila - Malunde1 blog

Wananchi katika Halmashauri ya wilaya ya Bukoba mkoani Kagera wamehimizwa kufuatilia miradi mbalimbali ikiwemo ya maji inayoletwa katika maeneo ya ili kujua bajeti ya miradi hiyo na ukidhi wa viwango jambo litakalosaidia kutopokea miradi hewa.

Kauli hiyo imetolewa leo na Shakira Omary ambaye ni Mratibu wa shirika lisilo la kiserikali la  Faraja For Hope And Development Organisation linalojihusisha na uwajibikaji, ufuatiliaji wa jamii katika sekta ya maji lililopo katika kata ya Nshambya manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera.

Omary amesema  wananchi ni chachu ya maendeleo ya taifa hivyo wananchi wanapaswa kufuatilia kila miradi iliyopo katika maeneo yao kwa sababu mwananchi anachangia kwa asilimia mia moja katika miradi hiyo.

Amesema baadhi ya wananchi wamekuwa woga katika kuhoji viongozi wanawaletea miradi ya maji jambo linasababisha kupokea miradi isiyokuwa na viwango mwisho wa siku kuwa na miradi hewa kutokana na hali hiyo amewataka kuwa huru kuhoji na kujua bajeti ya miradi na jinsi inavyotunzwa.

Mwezeshaji kutoka katika shirika hilo Andochius Kamuhabwa, amesema kuwa jambo linalofanyika kwa sasa ni kuona kwanini miradi mingi ya maji inaanzishwa au kuwekezwa kwa gharama kubwa lakini baada ya siku haifanyi kazi.



Kamuhabwa amesema matarajio yao ni kufika vijijini na kuangalia baadhi ya miradi iliyopo kama inafanya kazi vizuri na kwa ufanisi na kama haifanyi kazi vizuri lazima zitazamwe changamoto zinaifanya baadhi ya miradi hiyo kutokamilika.


Hata hivyo wananchi hao wamehimiza kuvitunza vyanzo vya maji kwa kuwa wafuatiliaji katika miradi hiyo.


Shirika hilo linahudumia kata 6 katika halmashauri ya wilaya ya Bukoba ambazo ni Ibwera, Katoma, Katoro, Katerero, Maruku,na Kemondo. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527