MWALIMU ATIWA MBARONI KWA RUSHWA YA LAKI MOJA


Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa Temeke, imemkamata Mwalimu Mkuu wa Shule ya Awali na Msingi Real Hope iliyopo Mbagala Majimatitu, Dar es Salaam, Ayubu Mtondo kwa kosa la  kuomba na kupokea rushwa.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Naibu Mkuu wa Takukuru, Ramadhani Ndwatah, alisema mwalimu huyo alipokea Sh 100,000 ili kumsaidia kumrudisha kazini mtumishi mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa.

Ndwatah alisema Februari 28, mwaka huu, saa 11 jioni,  mwalimu huyo akiwa ofisini kwake, alipokea fedha za mtego ili aweze kumsaidia mtumishi wake aliyesimamishwa kazi kurudi kazini.

Alisema uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo umekamilika na mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani na kufunguliwa mashtaka kwa kosa la kushawishi kuomba na kupokea rushwa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527