MLIPUKO WA LORI LA MAFUTA WASABABISHA VIFO VYA WATU WENGI UGANDA | MALUNDE 1 BLOG

Monday, August 19, 2019

MLIPUKO WA LORI LA MAFUTA WASABABISHA VIFO VYA WATU WENGI UGANDA

  Malunde       Monday, August 19, 2019

Watu kadhaa wamekufa baada ya lori la mafuta kulipuka jana kwenye mtaa wa Rubirizi, magharibi mwa Uganda.

Msemaji wa polisi wa mkoa wa Great Bushenyi, Marshal Tumusiime, amesema, mlipuko huo ulitokea baada ya lori hilo kupinduka, kulipuka na kuwaka moto katika kituo cha biashara cha Kyambura, kando na Barabara kuu ya Kasese-Mbarara.


Moto huo ulienea katika nyumba na maduka kadhaa na kuteketeza vitu. Onesmus Nkesiga ambaye duka lake lilikumbwa na moto huo, alisema  amepoteza bidhaa zenye thamani ya USh 20 milioni.

Wazima moto ambao walifika katika eneo hilo saa moja baada ya tukio, wameokoa vitu kadhaa kwenye baadhi ya maduka.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post