MBUNGE WA KISHAPU SULEIMAN NCHAMBI AWAONDOLEA HOFU YA MAJI WANANCHI

Wananchi katika wilaya ya Kishapu wanatarajiwa kunufaika na mradi wa maji safi na salama kutoka ziwa Victoria mradi ambao utawasaidia kuondokana na adha ya ukosefu wa huduma ya maji inayowakabili hivi sasa.

Hayo yamesemwa jana na Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mheshimiwa Suleiman Nchambi wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM, katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Somagedi.

Amesema kuwa tayari usanifu na michoro yote imeshakamilika hivyo ameiomba serikali itoe fedha kwaajili ya kukamilisha zoezi la usambazaji wa maji katika wilaya hiyo.

Kwa upande wake Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema kuwa atalifikisha suala hilo kwa Waziri Mkuu ili fedha zitolewe kwa ajili ya kukamilisha usambazaji wa maji safi na salama kwa matumizi ya wananchi na kwamba suala hilo ni muhimu hivyo litakekelezwa kwa haraka.
Na Annastazia Paul - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post