KENYA YAISHINDA DJIBOUTI NA KUPATA KURA YA UMOJA WA AFRIKA


Kenya imeishinda Djibouti na kupata kura ya Umoja wa Afrika ambayo inatarajiwa kuongeza chachu ya kampeni ya nchi hiyo kuwa mjumbe asiye wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.


Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo imesema, Kenya imepata kura 37 dhidi ya 13 za Djibouti wakati wa uchaguzi ulioandaliwa na Kamati ya Kudumu ya Wawakilishi ya Umoja wa Afrika uliofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Kenya inatarajiwa kuungana na Niger na Tunisia ambazo zilichaguliwa mwezi June kuwa wajumbe wasio wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ameupongeza Umoja wa Afrika kwa kuidhinisha nia ya Kenya ya kuwa na nafasi kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na kuzitaka nchi nyingine wanachama wa Umoja huo kuunga mkono kenya kupata nafasi hiyo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post