Picha : MAELFU WAKIONGOZWA NA ASKOFU MAGWESELA WAJITOKEZA UFUNGUZI WA KANISA JIPYA AICT KAHAMA MJINI

Askofu Mkuu wa Kanisa la AICT nchini,Musa Masanja Magwesela amefungua rasmi nyumba mpya ya kuabudia (kanisa la jipya AICT Kahama Mjini) lililogharimu zaidi ya shilingi milioni 900.

Ufunguzi wa kanisa hilo bora na la kisasa lililopo Nyihogo Mjini Kahama umefanyika leo Jumapili Agosti 25,2019 na kuhudhuriwa na maelfu ya viongozi,waumini na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga.

Akizungumza wakati wa kuweka wakfu na kufungua jengo hilo jipya,Askofu Magwesela alisema ni jengo bora na la kisasa huku akiwasisitiza waumini na kutumia jengo hilo kumwabudu Mungu.

"Kwa heshima ya Mungu nalifungua na kuliweka wakfu jengo hili. Nyumba hii ni kwa ajili ya ibada pekee,naomba mlitumie kwa maksudi yaliyokusudiwa",amesema. 

Akisoma taarifa ya ujenzi,Katibu wa Kanisa la AICT Kahama Mjini,Charles Pambe amesema kanisa la AICT Kahama Mjini limeanzishwa tarehe 15 Novemba,1975 na mpaka sasa limefungua Pastoreti tisa mjini Kahama na Pastoreti mama ya Kahama,Mlima Sayuni,Mhongolo,Mhungula,Nyakato,Lugela,Majengo,Mbulu na Mwendakulima.

Amesema wamejenga jengo jipya kisasa la kuabudia lililotokana na michango ya waumini ambapo lina mahitaji muhimu ikiwa ni pamoja na ofisi sita,vyoo,sehemu ya kubatizia na maombi ya faragha,mabenchi,meza hivyo mpaka jengo linafunguliwa limegharimu jumla ya shilingi 902,397,070/=.

Amebainisha kuwa mbali na kujenga kanisa jipya lenye uwezo wa kubeba watu 850 pia wamejenga nyumba ya kisasa ya Mwinjilisti,madarasa mawili na ofisi zake,bwalo la kulia chakula na kanisa linaendelea na utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule ya msingi 'English Medium School',ujenzi wa shule ya sekondari na zahanati na ukamilishaji wa hosteli ya kanisa.

ANGALIA PICHA HAPA 
Askofu Mkuu wa Kanisa la AICT nchini,Musa Masanja Magwesela akiendesha ibada ya kufungua na kuweka wakfu jengo jipya la kuabudia katika kanisa la AICT Kahama Mjini leo Jumapili Agosti 25,2019. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Askofu Mkuu wa Kanisa la AICT nchini,Musa Masanja Magwesela akiendesha ibada ya kufungua na kuweka wakfu jengo jipya la kuabudia katika kanisa la AICT Kahama Mjini.
Maaskofu wa kanisa la AICT wakiendelea na ibada ya ufunguzi na uwekaji wakfu jengo jipya la kanisa la AICT Kahama Mjini. Aliyeshikilia kipaza sauti ni Askofu wa Dayosisi ya Shinyanga, Zakayo Bugota.
Muonekano wa jengo jipya la kanisa la AICT Kahama Mjini.

Muonekano wa jengo jipya la kanisa la AICT Kahama Mjini.
Askofu Mkuu wa Kanisa la AICT nchini,Musa Masanja Magwesela akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa  jengo jipya la kuabudia katika kanisa la AICT Kahama Mjini.
Askofu Mkuu wa Kanisa la AICT nchini,Musa Masanja Magwesela akikata utepe wakati wa kufungua jengo jipya la kuabudia katika kanisa la AICT Kahama Mjini.
Askofu Mkuu wa Kanisa la AICT nchini,Musa Masanja Magwesela akifungua jengo jipya la kuabudia katika kanisa la AICT Kahama Mjini.
Askofu Mkuu wa Kanisa la AICT nchini,Musa Masanja Magwesela akifungua mlango kuingia ndani ya jengo jipya la kuabudia/kanisa la AICT Kahama Mjini.
Katibu wa Kanisa la AICT Kahama Mjini,Charles Pambe akisoma taarifa ya ujenzi wa kanisa jipya la AICT Kahama Mjini ambalo limegharimu jumla ya shilingi milioni 900.
Katibu wa Kanisa la AICT Kahama Mjini,Charles Pambe akisoma taarifa ya ujenzi wa kanisa jipya la AICT Kahama Mjini ambalo limegharimu jumla ya shilingi milioni 900.
Askofu Mkuu wa Kanisa la AICT nchini,Musa Masanja Magwesela  akizungumza wakati wa kufungua kanisa jipya la AICT Kahama Mjini na kuwasisitiza waumini kutumia kanisa hilo kumwabudu Mungu pekee.
Askofu Mkuu wa Kanisa la AICT nchini,Musa Masanja Magwesela  akizungumza wakati wa kufungua kanisa jipya la AICT Kahama Mjini.
 Askofu wa Dayosisi ya Shinyanga, Zakayo Bugota akizungumza wakati wa ufunguzi wa kanisa jipya la AICT Kahama Mjini.
Askofu wa Kanisa la AICT Dayosisi ya Tabora, Silasi Kezakubi akiweka wakfu benchi katika kanisa jipya la AICT Kahama Mjini.
Askofu Mkuu wa Kanisa la AICT nchini,Musa Masanja Magwesela  akizungumza baada ya kufungua kanisa jipya la AICT Kahama Mjini.
Viongozi mbalimbali wa Kanisa la AICT wakiwa kanisani wakati wa kufungua kanisa jipya la AICT Kahama Mjini.

Maaskofu wakiwa wamekaa jukwaa kuu wakati wa ibada ya Jumapili baada ya kufungua kanisa jipya la AICT Kahama Mjini.
 Askofu wa Kanisa la AICT Dayosisi ya Tabora, Silasi Kezakubi akizungumza kwenye ibada baada ya ufunguzi wa kanisa jipya la AICT Kahama Mjini.
Kwaya ya AICT Chang'ombe wakimsifu Mungu wakati wa ufunguzi wa kanisa jipya la AICT Kahama Mjini.

Katibu Mkuu wa kanisa la AICT, Josephet Mtebe akizungumza wakati wa ibada ya Jumapili katika kanisa la AICT Kahama Mjini

Askofu Mkuu wa Kanisa la AICT nchini,Musa Masanja Magwesela akihubiri katika ibada ya Jumapili baada ya kufungua jengo jipya la kuabudia katika kanisa la AICT Kahama Mjini.

Askofu Mkuu wa Kanisa la AICT nchini,Musa Masanja Magwesela akihubiri katika ibada ya Jumapili baada ya kufungua jengo jipya la kuabudia katika kanisa la AICT Kahama Mjini.

Wachungaji na wageni mbalimbali wakiwa kwenye ibada ya Jumapili katika kanisa la AICT Kahama Mjini.

Waumini wa kanisa la AICT na wageni mbalimbali wakiwa kwenye ibada baada ya ufunguzi wa kanisa jipya la AICT Kahama Mjini.

Kwaya akina mama wakimsifu Mungu kwa nyimbo.

Kahama Town Choir wakimsifu Mungu kwa nyimbo.

Kahama Vijana Choir wakimsifu Mungu kwa nyimbo.

Waumini wa kanisa la AICT wakiwa kwenye ibada baada ya ufunguzi wa kanisa jipya la AICT Kahama Mjini.

Ibada inaendelea.

Wageni mbalimbali waliohudhuria ibada ya Jumapili baada ya ufunguzi wa kanisa jipya la AICT Kahama mjini wakiendelea na Harambee kuchangia ujenzi wa shule ya kanisa hilo ambapo kiasi cha shilingi milioni 30 zinahitajika ili kukamilisha ujenzi huo.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527