HALMASHAURI YA BUKOBA YAKUSANYA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI MOJA MWAKA WA FEDHA 2018/2019


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Murshid Hashim Ngeze.
Na Lydia Lugakila - Malunde 1 blog
Zaidi ya shilingi bilioni moja na Milioni mia tatu zimekusanywa na Halmashauri ya wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera Kwa Mwaka fedha 2018/2019 ambazo ni zaidi ya asilimia 97 za mapato kwa mwaka mzima.

Akizungumza leo Jumamosi Agosti 31,2019  katika kikao cha halmashauri hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo kilicholenga kufunga robo ya nne ya mwaka wa fedha 2018/2019,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Murshid Hashim Ngeze,amesema  mafanikio hayo yamekuja kutokana na kasi ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kusimamia vizuri rasilimali mbalimbali za nchi.

"Mafanikio hayo yamekuja kutokana na kasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DkT. John Pombe Magufuli katika kusimamia vizuri rasilimali mbalimbali za nchi na ndo sababu kila kiongozi amewajibika kwa nafasi yake kuanzia ngazi ya juu mpaka ya chini kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania wote ujumla",ameeleza.
 

Ngeze amesema Halmashahuri hiyo imepiga hatua kubwa na kudai kuwa wakati wanaingia madarakani walikuwa wakikusanya zaidi ya shilingi milioni mia sita kwa mwaka lakini mpaka sasa wamevuka malengo kwa 100% kwa miaka minne wakiwa kwenye uongozi.

"Ni jambo la kumshukuru mungu nikikumbuka tulipoanzia hadi sasa ni hatua kubwa hii ni kutokana na juhudi kubwa za Rais wetu za mapambano yenye kuleta maendeleo amesema’’ ,amesema.


Mwenyekiti huyo ambaye pia ni diwani wa kata ya Rukoma amesema tayari ujenzi wa shule ya sekondari umeanza kwenye kata ya Rukoma ili kutatua changamoto inayowakabili wanafunzi wa kata hiyo wanaohangaika kufuata huduma ya elimu umbali mrefu na kulazimika kutembea takribani kilometa 38.

Hata hivyo Ngeze ametoa wito kwa wananchi kufanya kazi kwa bidii ili kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post