WEMA SEPETU AACHIWA HURU NA KISHA KUKAMATWA TENA

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu, lakini dakika chache baadaye askari magereza walimkamata tena.

Malkia huyo wa filamu anakabiliwa na kesi ya kusambaza picha zinazodaiwa kuwa za ngono mtandaoni.

Wema ambaye anakabiliwa na shitaka moja la kuchapisha video na picha za faragha na kuzisambaza katika mtandao wa Instagram kinyume cha sheria.

Ikumbukwe kuwa June 24, mahakama hiyo ilimuonya kutokiuka masharti ya dhamana la sivyo mahakama itamfutia dhamana yake.

Hakimu Mkazi Mkuu, Maira Kasonde alimuachia huru mshtakiwa huyo kwa sheria ya kifungu cha 225(5), cha mwenendo wa mashtaka ya makosa ya jinai.

Katika kesi ya msingi Wema anadaiwa kutenda kosa hilo Oktoba 15, 2018, katika maeneo ya jiji la Dar Es Salaam, alirekodi video ya ngono na kuisambaza katika ukurasa wake wa kijamii wa Instagram.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527