WAFANYABIASHARA WASHAURIWA KUTUMIA MAONYESHO YA BIASHARA YA KIMATAIFA (SABASABA) KUTANGAZA BIDHAA ZAO | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, July 3, 2019

WAFANYABIASHARA WASHAURIWA KUTUMIA MAONYESHO YA BIASHARA YA KIMATAIFA (SABASABA) KUTANGAZA BIDHAA ZAO

  Malunde       Wednesday, July 3, 2019

Wafanyabiashara nchini wameshauriwa kutumia Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) kama uwanja wa kutangaza bidhaa zinazozalishwa na viwanda vyao.


Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan jana Jumanne Julai 2, wakati akizindua maonyesho hayo katika viwanja vya Sababa jijini Dar es Salaam, katika maonyesho hayo yaliyobeba kauli mbiu isemayo ‘usindikaji wa mazao ya kilimo kwa maendeleo endelevu’.

Mama Samia alisema maonyesho hayo ambayo yamejizolea umaarufu Afrika Mashariki na Kati hutembelewa na watu wengi kutoka ndani na nje ya nchi hivyo yakitumika vizuri ni sehemu sahihi ya wafanyabiashara kupanua wigo wao kibiashara.

Katika hatua nyingine Mama Samia amewataka wakulima kulima mazao kwa wingi kwani Serikali inaendelea kujenga viwanda ambavyo malighafi yake itatoka hapa nchini hususani katika sekta ya kilimo.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post