LUGOLA AAGIZA MAGARI YALIYOKOPESHWA KWA WATUMISHI WA NIDA YAREJESHWE HARAKA | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, July 3, 2019

LUGOLA AAGIZA MAGARI YALIYOKOPESHWA KWA WATUMISHI WA NIDA YAREJESHWE HARAKA

  Malunde       Wednesday, July 3, 2019

Serikali kupitia Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania, Kangi Lugola ameagiza waliokuwa watumishi watatu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), kuyarudisha magari aina ya Toyota Land Cruiser wanayoyamiliki kinyume cha sheria.

Waziri Lugola alitoa kauli hiyo Jumanne hii katika kikao chake na viongozi wa ngazi ya juu wa Nida.

Alisema miongoni mwa watumishi wanaomiliki magari hayo ni pamoja na aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa Nida, Dickson Maimu.

Alimuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dk Arnold Kihaule kushughulikia suala hilo hadi ifikapo jana jioni yawe yamerejeshwa katika maegesho ya ofisi za Nida.

Kikao hicho kilifanyika Jijini Dodoma, na kilikuwa kinapokea taarifa ya idadi ya mali za Nida zilizopo na zilizopokelewa na mwenendo wa matumizi yake.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post