TETESI ZA SOKA ULAYA JUMATANO


Atletico Madrid wanataka kumsajili Alexandre Lacazette kuchukua nafasi ya mshambuliaji Antoine Griezmann, 28 ambaye anaelekea Barcelona. (Mirror)
United watalazimika kilipa zaidi ya pauni milioni £90 kumnunua beki wa Leicester City na England, Harry Maguire - hatua itakayomfanya kuwa nyota huyo wa miaka 26 kuwa mlinzi ghali zaidi . (Telegraph)

United pia imetuma maombi ya kumnasa kiungo wa kati wa Uhispania na Dinamo Zagreb-Dani Olmo, 21. (Mail)

Real Madrid wana mpango wa kumjumuisha mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, 29, katika mkataba utakaowawezesha kumnunua kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 26. (Mail)

Mlinzi wa Bournemouth na Uholanzi Nathan Ake, 24, huenda akatia saini mkataba wa kujiunga na Manchester City mhumu ujao. (L'Equipe, via Manchester Evening News)

Crystal Palace wanafanya kila juhudi kuhakikisha hawataiuzia Arsenal winga wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 26, na wana hasiri kwa sababu wanaamini Gunners wanafanya kusudi ili kumvuruga akili mchezaji huyo. (Mirror)
Winga wa Barcelona na Ufaransa Ousmane Dembele, 22, hana mpango wa kuondoka Nou Camp msimu huu wa joto licha ya vilabu vikubwa Ulaya ikiwa ni pamoja na Liverpool na Bayern Munich kuonesha nia ya kutaka kumsajili. (L'Equipe)

West Ham wanahofia huenda wakakosana na mshambulizi wa Austria Marko Arnautovic, 30, wasipomuuza. (Mirror)

Barcelona wako tayari kupokea maombi ya kumnunua mlinzi wa kati wa miaka 25-Mfaransa Samuel Umtiti, ambaye analengwa na Manchester United. (Sport, via Mirror)Umtiti alijiungana Barcelona mwaka 2016

Chelsea wameafikiana kuhusu mkataba mpya wa muda mrefu na kiungo wa kati wa England Ruben Loftus-Cheek, 23. (Telegraph)

Mlizi wa Arsenal Mfaransa Laurent Koscielny, 33,ananyatiwa na Bordeaux. (L'Equipe)

CHANZO.BBC SWAHILI.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527