Uhuru Kenyatta atengua uteuzi wa Waziri wa Fedha, amteua Waziri wa Kazi kushika nafasi yake | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, July 24, 2019

Uhuru Kenyatta atengua uteuzi wa Waziri wa Fedha, amteua Waziri wa Kazi kushika nafasi yake

  Malunde       Wednesday, July 24, 2019
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ametengua uteuzi wa Waziri wa Fedha Henry Rotich na kumteua Waziri wa Kazi, Ukur Yattan kushika nafasi yake.

Rais Kenyatta ametengua uteuzi huo leo Jumatano Julai 24, ikiwa ni siku moja tangu Rotich apandishwe kizimbani akikabiliwa na tuhuma za ufisadi kufuatia sakata la ujenzi wa mabwawa ya Kimwarer na Arror uliogharimu shilingi bilioni 19 za Kenya.

Rotich alikamatwa Julai 23, kufuatia Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) nchini humo, Noordin Haji, kutoa agizo la kumkamata pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Thugge Kamau na maafisa wengine wa Serikali kwa tuhuma za kufanya udanganyifu na kushindwa kutii muongozo wa unaotumika katika upatikanaji wa kandarasi.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post