TETESI ZA USAJILI ULAYA JUMANNE | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, July 23, 2019

TETESI ZA USAJILI ULAYA JUMANNE

  kisesa       Tuesday, July 23, 2019

Uwezekano wa Real Madrid kumsajili kiungo wa kati wa Manchester United Mfaransa Paul Pogba, 26, utategemea kuondoka kwa mshambuliaji wa kimataifa wa Wales Gareth Bale, 30, kuondoka klabu hiyo ya Uhispania. (AS)

Bale, ambaye anapokea pauni 550,000 kwa wiki katika uga wa Bernabeu, ambako ana mkataba wa hadi mwaka 2022, anataka marupu rupu yanayolingana na wachezaji wakuu duniani kuondoka Real Madrid, kinasema chanzo cha habari kilicho na uhusiano wa karibu na nyota huyo. (Sky Sports)

Barcelona wako tayari kufanya mazungumzo na Lionel Messi, 32, kurefusha mkataba wa nyota huyo raia wa Argentina kwa miaka minne zaidi. (ESPN)Lionel Messi ameshinda mataji manne ya Ulaya

Tottenham wanajiandaa kutumia tena kitita kikubwa cha fedha wiki hii kukamilisha usajili wa kiungo wa kati wa Real Betis na Argentina Giovani lo Celso, 23, pamoja na mlinzi wa wa chini ya miaka 21 wa Fulham na England, Ryan Sessegnon, 19. (Mirror)Giovani Lo Celso aliifungia Real Betis mabao 16 msimu uliopita

Fulham wanataka pauni milioni 40 kumuachilia Sessegnon lakini Spurs wanamini wanaweza kuafikiana kwa mkataba wa karibu pauni milioni 25 kumnasa mchezaji huyo ambaye amesalia na mwaka mmoja kukamilisha mkataba wake Craven Cottage.

Sessegnon pia anapania kusalia London, japo vilabu vingine vikubwa kama vile Manchester United, Paris St-Germain, Juventus na Borussia Dortmund pia vimekuwa vikimfuatilia. (London Evening Standard)Ryan Sessegnon (kulia)

Toby Alderweireld anatarajia kubaka Tottenham, licha ya Roma kuhusishwa na uhamisho wa mlinzi huyo wa miaka 30 raia wa Ubelgiji ambaye masharti ya mkataba wake yanasema lazima auzwe ikiwa klabu inayotaka kumnunua ina uwezo wa kufikia ada ya pauni milioni 25 kufikia Alhamisi wiki hii. (Telegraph)

Mkufunzi wa zamani wa Chelsea Maurizio Sarri anataka kumjumuisha mlinzi wa Tottenham Danny Rose, 29, katika kikosi chake cha Juventus. (Mail)Danny Rose

Atletico Madrid huenda wakaelekeza juhudi zao katika harakati ya kumsaka mchezaji nyota wa Real Madrid MColombia James Rodriguez, 28, badala ya kumsajili kiungo wa kati wa Tottenham Christian Eriksen, 27. (Marca)

Antoine Griezmann, 28, ameashiria kuna ''uwezekano'' wa kujiunga na Manchester United siku zijazo huku mchezaji huyo mpya wa Barcelona akielezea azma yake ya kucheza na mchezaji mwenza wa Ufaransa na mshambuliaji wa Arsenal Alexandre Lacazette, 28, katika soka ya kiwango cha vilabu. (Goal.com)Antoine Griezmann

Kipa wa Manchester United David de Gea, 28, anajiandaa kutia saini mkataba ulioboreshwa wa thamani ya pauni milioni 117 ambao huenda ukaendelea hadi mwaka 2025, na pia anataka kuwa nahodha Old Trafford. (Manchester Evening News)

Mlinzi wa England Harry Maguire, 26, hana mpango wa kuhama Leicester licha ya tetesi zinazomhusisha na uhamisho wa Manchester United. (Leicester Mercury)Harry Maguire

Juventus wako tayari kuizia Manchester United mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala, 25, msimu huu wa joto, bei yao ya kati ya £70m na pauni milioni 90 ikifikiwa. (Mail)

Mshambuliaji wa zamani wa Crystal Palace Clinton Morrison anatarajia mshambuliaji wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 26, atasalia katika uwanja wa Selhurst Park msimu huu, licha ya mchezaji huyo kunyatiwa na Arsenal Bayern Munich. (Talksport)Zaha aliifungia Palce mabao 10 katika msimu wa mwaka 2018-19

Arsenal wako mbali sana kufikia kiwango cha pauni milioni 80 zinazoitishwa na Crystal Palace kumwachilia Zaha, huku wasimamizi wa Selhurst Park wakipuuzilia mbali ofa za hivi karibuni za kutaka kumnunua kiungo huyo. (Independent)


Wolves wako tayari kuweka dau la pili la kumnunu a mlinzi wa Olympiacos Pape Abou Cisse, 23. (Sport Witness, via Birmingham Mail)

Kiungo wa kati wa Brighton Taylor Richards, 18, anasema haikuwa rahisi kufanya uamuzi wa kuondoka Manchester City kwenda Seagulls. (Argus)

CHANZO.BBC SWAHILI
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post