TETESI ZA SOKA ULAYA JUMANNEKocha wa United, Ole Gunnar Solskjaer amewaambia wakuu wa klabu hiyo kumsajili kiungo wa kati wa Newcastle Muingereza Sean Longstaff, 21, kwa mshahara wa pauni milioni 21 kwa wiki. (Star)
Barcelona wako tayari kulipa euro milioni 100 ya kumwezesha mshambuliaji wa Inter Milan Muargentina Lautaro Martinez, 21 kuondoka klabu hiyo kabla mkataba wake kukamilika. (Corriere dello Sport - in Italian)

Ofa ya Manchester United ya £31m ya kumnunua kiungo wa kati wa Ureno Bruno Fernandes, 24, imekataliwa na Sporting Lisbon. (Gazzetta dello Sport, via Express)

Ni rasmi sasa Meneja wa Derby County Frank Lampard amerejea Chelsea baada ya mchezaji huyo wa zamani wa blues kutia saini mkataba pauni milioni 4 kwa mwaka. (Mail)Bruno Fernandes

Kocha wa zamani wa Newcastle Rafael Benitez amekubali kujiunga klabu ya Uchina ya Dalian Yifang kwa mkataba wa thamani ya euro milioni 12 kwa mwaka baada ya kuondoka St James Park. (Sky Sports)

Rams wanajiandaa kufanya mazungumzo na kiungo wa kati wa zamani wa Uholanzi Phillip Cocu wiki hii kabla ya Lampard kuondoka.

Cocu alitupwa nje na kocha wa Fenerbahce mwezi Octoba. (Telegraph)

Kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 26, amekuwa akifanya mazoezi mjini New York licha ya wachezaji wenzake kurejea kambini kwa mazoezi ya kabla ya msimu mpya kuanza. (Sun)
Paul Pogba

Arsenal wanashauriana na mshambuliaji wa Algeria, Yacine Brahimi 29 ambaye yuko huru na kujiunga na klabu nyinhine baada ya kuhama Porto. (Sky Sports)

Gunners pia wamepewa nafasi ya kusaini mshambuliaji wa Lyon na Ufaransa Nabil Fekir - kwa uero milioni 30. (Mirror)

Winga wa Manchester City Mjerumani Leroy Sane ameangaziwa katika uzinduzi wa jezi za msimu wa mwaka 2019-20, licha ya tetesi kuwa Bayern Munich wamekuwa wakimnyatia nyota huyo wa miaka 23. (Express)Leroy Sane aliisaidia Ujerumani kufuzu kwa nusu fainali ya michuano u a kombe la Euro 2016

Crystal Palace wanamtaka mlinzi wa Arsenal Muingereza Carl Jenkinson, 27, kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na mlinzi Aaron Wan-Bissaka, ambaye amejiunga na Manchester United. (Sun)

Gunners wanajiandaa kuweka dau la pauni milioni 12 kumnunua mshambuliaji wa Hull City wa miaka 22-year- Muingereza Jarrod Bowen. (Sun)

Mshambuliaji wa Uholanzi Hossein Zamani, 16, amevifahamisha villabu vya Manchester United, Manchester City na AC Milan kuwa aAjax. (Mail)

CHANZO.BBC SWAHILI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post