TAIFA STARS,HARAMBEE STARS WAGONGWA TATU TATU


Sadio Mane aliifungia Senegal bao moja na kuisaidia timu yake kuchukua nafasi ya pili katika kundi C baada ya kuilaza Kenya 3-0 na kufuzu miongoni mwa timu 16 bora.
Penalti ya mshambuliji huyo wa liverpool iliokolewa na kipa Patrick Matasi wa Kenya kabla ya Senegal kufunga goli lake la kwanza kupitia Ismaila Sarr.

Mane baadaye alifunga penalti nyengine baada ya Philemon Otieno kupewa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Sarr kunako dakika za mwisho.

Wakati huohuo kiungo wa kati wa Napoli Adam Ounas alifunga magoli mawili na kutoa pasi nzuri iliosababisha goli la tatu katika mechi yake ya kwanza katika michuano ya Afcon na kuisaidia Algeria kupata ushindi wa tatu mfululizo dhidi ya Tanzania.
Ounas alimpigia pasi murua mshambuliaji wa Leicester Islam Slimani katika bao la kwanza kabla ya ya kufunga magoili mawili katika kipindi cha kwanza kilichotawaliwa na Mbweha hao wa jangwani.

Algeria ambao walimaliza kileleni mwa kundi C walikuwa tayari wamefuzu miongoni mwa timu 16 bora baada ya kushinda mechi za kwanza mbili.

Sasa watacheza dhidi ya timu bora katika nafasi ya tatu katika raundi inayofuata.

Huku ikiwa tayari imefuzu, mkufunzi wa Algeria Djamel Belmadi alikifanyia kikosi chake cha kwanza mabadiliko tisa akimwanzisha Slimani ambaye amekosa kuchezeshwa kutokana na umahiri wa mshambuliaji Baghdad Bounedjah.
Slimani alifunga goli la kwanza na lake la kimataifa la 27 baada ya dakika 30 katika mechi yake ya 31 kufuatia pasi nzuri kutoka kwa Ounas.

Na katika mechi dhidi ya Senegal na Kenya , mabingwa hao wa afrika magharibi sasa watachuana na Uganda tarehe 5 mwezi Julai.

Kenya inaweza ikafuzu kama timu ya tatu bora ikitegemea matokeo katika mechi ya mwisho katika kundi E and F.

Hatahivyo matokeo ya Jumatatu yanamaanisha kwamba DR Congo inaweza kufuzu kutoka kundi A ikiwa na goli moja zaidi.
CHANZO.BBC SWAHILI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527