RAIS MAGUFULI AELEZA SABABU YA KUMUONDOA JANUARY MAKAMBA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, amebainisha baadhi ya matatizo yaliyokuwa yakipatikana kwenye Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, ikiwemo ucheleweshwaji wa utoaji wa vibali kutoka NEMC, pamoja na kupokea malalamiko ya wawekezaji kuhusu taasisi hiyo.


Akizungumza wakati akiwaapisha Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, George Simbachawene na Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, leo Julai 22, 2019, Ikulu jijini Dar es salaam, Rais amesema kuna baadhi ya wawekezaji walikuwa wakikwamishwa na NEMC.

Magufuli amesema kuwa, "nataka kusiwe na ucheleweshaji wa kutoa vibali vya NEMC kwa wawekezaji wa Viwanda hapa Tanzania, vibali hivi vitoke kwa wakati kwa sababu tunahitaji viwanda ikiwezekana wawekeze kwanza na vibali vije baadaye."

Audha Rais ameongeza kuwa "Nakumbuka suala la mifuko ya plastiki lilichukua karibia miaka 4, nilisaini lakini halikutekelezwa mpaka hapa mwishoni nilitoa amri ya lazima, ndiyo likatekelezwa." ameongeza Rais Magufuli.

Julai 21, 2019 Rais Magufuli alifanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri, kwa kumuondoa Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba, na kumteua George Simbachawene kuongoza Wizara hiyo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527