RAIA WA MISRI KORTINI KWA TUHUMA ZA KUTOROSHA MADINI YENYE THAMANI YA MILIONI 12


Hany Ahmed (27)  ambaye ni raia wa Misri amefikishwa  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka moja la kutorosha madini aina ya diamond  yenye thamani zaidi ya Sh. Milioni 12.


Akisoma hati ya mashtaka  jana July 16, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba,  Wakili wa Serikali Wankyo Simon alidai,  Julai 10, mwaka huu huko katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, wilaya ya Ilala jijini  Dar es Salaam mshtakiwa  alikutwa akisafirisha madini ya diamond yenye uzito wa carats 11:12 ambayo yana thamani ya Dora za Kimarekani 5,238 sawa na Sh. 12,050,131bila ya kuwa na kibali.

Hata hivyo, mshtakiwa hakuruhusiwa kujibu chochote kwa sababu mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi. 

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na  kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 30, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa, mshtakiwa amerudishwa rumande.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post