POLISI PWANI YAUA MAJAMBAZI WANNE BAADA YA MAJIBIZANO YA RISASI | MALUNDE 1 BLOG

Friday, July 12, 2019

POLISI PWANI YAUA MAJAMBAZI WANNE BAADA YA MAJIBIZANO YA RISASI

  Malunde       Friday, July 12, 2019
Na Mwamvua Mwinyi,kibaha Vijijini
JESHI la Polisi Mkoani Pwani, limefanikiwa kuua majambazi wanne katika tukio la majibizano ya risasi baina ya polisi na majambazi hayo huko eneo la Kwala , Wilaya ya Kipolisi Mlandizi.

 
Kamanda wa polisi mkoani hapa,Wankyo Nyigesa alisema, tukio hilo la kuuawa kwa majambazi hayo limetokea jana majira ya saa 8 mchana baada ya taarifa kulifikia Jeshi la Polisi kuwa wapo watu wamepanga kwenda kuvamia na kupora fedha ambazo zilikuwa zimepangwa kwenda kulipwa kwa wanaojenga Bandari Kavu ya Kwala.

“Ndipo Jeshi la Polisi Mkoani hapa tuliweka mtego na majambazi hao kujikuta wakinasa na kuanzisha majibizano ya risasi na kupelekea majambazi wanne kati ya sita wanaodhaniwa kuwepo kupoteza maisha”alieleza Wankyo.

Hata hivyo majambazi wawili walitoweka eneo la tukio kwa kutumia gari lingine na msako wa kuwatafuta bado ungali ukiendelea.

Wankyo alifafanua, katika tukio hilo  majambazi hao wamekutwa wakiwa na bunduki mbili aina ya pump action, radio call moja, hirizi, dawa za kupulizia watu, kamba za kufungia watu na, plasta za kuziba watu midomoni.

Vitu vingine ni pamoja na leseni za udereva, vitambulisho mbalimbali vya uraia, kadi ya bima ya afya, koti, kaniki, kanzu, suruali, kaptula .

Kamanda huyo alibainisha, miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospital ya rufaa ya mkoa ya Tumbi .


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post