NEW HOPE TANZANIA : CHAGUENI VIONGOZI WENYE HOFU YA MUNGU, WANAOJALI HAKI ZA WATOTO WA KIKE


Wakati Taifa linajiandaa kwenda katika Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa, Wito umetolewa kwa wananchi kuhakikisha wanatumia haki yao ya msingi kwa kupiga kura za kuchagua Viongozi wenye hofu ya Mungu na wanaojali haki za watoto wa kike.

Hayo yameelezwa na Mratibu wa Shirika la utetezi wa haki za mtoto wa kike la New Hope Tanzania Bi. Elizabeth Ngaiza ambapo amesema katika Kampeni ya "Niache Nisome Kwanza" anayoendesha amebaini uwepo wa baadhi ya viongozi wa ngazi za mitaa wasiokuwa na weledi, wasiowajibika na hawawezi kusimama katika nafasi yao kutetea haki za mtoto wa kike.

Aidha Bi. Elizabeth Ngaiza amesema lengo la Kampeni ya "Niache Nisome Kwanza" ni kupambana na mimba za utotoni kwa mtoto wa kike na kuhakikisha anawekewa mazingira wezeshi ya kusoma pasipo changamoto wala vikwazo vyovyote.

Hata hivyo Bi.Ngaiza amewaomba wadau na wananchi kuendelea kumuunga mkono katika Kampeni hiyo ili kuhakikisha haki za watoto wa kike zinalindwa katika jamii.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527