MHANDISI WA MELI AJINYONGA BAHARINI KATIKATI YA SAFARI

Mhandisi msaidizi katika meli ya Mv Mapinduzi, Haji Abdalla Khatib (55) amefariki dunia baada ya kujinyonga wakati meli hiyo ilipokua inatoka Unguja kwenda Pemba.
Tukio hilo limetokea leo Jumatatu Julai 22, 2019, Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar, Mustafa Aboud Jume amesema baada ya kupata taarifa hiyo walilazimika kusitisha safari na kuamuru meli hiyo irudi Unguja.
Amesema Khatib amejinyonga katika chumba cha Injini, sehemu aliyokuwa anafanyia kazi na kwamba, hadi sasa bado hawafahamu sababu za kujinyonga kwake.
“Marehemu alikuwa fundi umeme wa miaka mingi tangu enzi za meli ya ukombozi, hivyo ni mtu muhimu sana,” amesema.
Amesema pamoja na hayo, uchunguzi wa kifo hicho umefanyika na tayari jeshi la polisi linaanza kazi zake mara moja kwa lengo la kubaini sababu zilizomfanya injinia huyo kujitoa uhai wake.
Na Muhammed Khamis, mwananchi 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527