MAREKANI YASEMA IMEIDUNGUA NDEGE ISIYO NA RUBANI YA IRAN


Raisi wa Marekani Donald Trump amesema jeshi la maji la Marekani limetungua ndege isiyo na rubani ya Iran katika eneo la mpaka kati ya ghuba ya uajemi na ghuba ya Oman.

Amesema meli ya jeshi lake ''ilichukua hatua'' siku ya Alhamisi baada ya ndege hiyo kusogea kwa takriban mita 914 karibu na chombo hicho.

Mwezi Juni, Iran iliangusha ndege ya kijeshi isiyo na rubani ya Marekani, na kusababisha hofu ya kutokea mzozo wa kijeshi.

Akizungumza Ikulu, Trump amesema ''Ninataka kuwajulisha kuhusu tukio lililotokea kwenye eneo la mpaka wa Hormuz leo lililohusisha meli yetu ya kijeshi.

"Chombo hicho kilichukua hatua ya kujilinda dhidi ya ndege isiyo na rubani ya Iran ambayo ilikuwa karibu sana hatua iliyokuwa ikitishia usalama wa meli na waliokuwa ndani ya meli hiyo. Ndege hiyo iliharibiwa mara moja''.

"Hili ni tukio miongoni mwa matendo mengine ya uchokozi unaofanywa na Iran dhidi ya meli zinazokuwa kwenye maji ya kimataifa. Marekani in haki ya kujitetea, na kutetea maslahi yake''.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527