IRAN YAKAMATA MELI YA KIGENI ILIYOBEBA SHEHENA YA MAFUTA


 Kikosi cha ulinzi ya mapinduzi cha Iran kimeikamata meli ya mafuta ya kigeni katika eneo la Ghuba na kuwakamata wafanyakazi wake 12, wakiwashutumu kwa kusafirisha mafuta kwa njia haramu, shirika la habari la Tasnim limeripoti.

Meli hiyo ilikuwa imebeba lita milioni moja za mafuta wakati ilipokamatwa wakati ikipita katika ujia wa maji wa Hormuz , kwa mujibu wa shirika la habari la Tasnim, ambalo halikusema ni taifa gani meli hiyo inatoka ama inatoa huduma kwa kampuni gani.

Eneo hilo la Ghuba ni moja kati ya maeneo muhimu ya njia za majini kwa ajili ya kusafirisha mafuta.

Eneo hilo limekuwa tete wakati hali ya wasi wasi ikiendelea kuongezeka kati ya Iran na Marekani kuhusiana na makubaliano ya nyuklia ya Iran yanayosambaratika na mataifa yenye nguvu duniani na hofu inaongezeka kuwa pande hizo mbili zinasogea karibu na makabiliano ya kijeshi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527