MAMBO SASA AMJIBU ZITTO KABWE SAKATA LA KUTEKWA RAIA WA KENYA | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, July 2, 2019

MAMBO SASA AMJIBU ZITTO KABWE SAKATA LA KUTEKWA RAIA WA KENYA

  Malunde       Tuesday, July 2, 2019

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam (SACP) Lazaro Mambosasa, amewataka watu wenye taarifa zitakazosaidia upatikanaji wa  Raphael Ongangi, waziwasilishe ofisini kwake ili zifanyiwe kazi.

Akizungumzia juu ya kauli zilizotolewa na kiongozi wa ACT Wazalendo,  Zitto Kabwe juu ya alipo Raphael,  kamanda amesema taarifa hizo  ni za mitandaoni, na kwamba wao hawafanyii kazi mambo ya mitandao.

“Hizo habari za mitandao kila mmoja anatoa anavyofikiria, cha msingi ambacho sisi tungeweza kukiona cha maana kama kuna jambo lolote lipelekwe kituo cha polisi, ofisi yangu ipo, kama kuna mtu ana taarifa alete". alisema Mambosasa.

Siku ya Julai Mosi, Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, aliahidi kuwasilisha ushahidi wa eneo alilowekwa Raphael, kuanzia siku ya kwanza alipotekwa hadi siku ya Jumamosi.

Raia huyo wa Kenya ambaye ana mke na watoto wawili, alitekwa Juni 24 maeneo ya Oyserbay Dar es salaam ambapo hadi sasa bado hajapatikana.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post