KUBENEA ATAKA WANAOSAMBAZA MAWASILIANO YA SIMU YA NAPE, MAKAMBA, KINANA WACHUKULIWE HATUA | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, July 23, 2019

KUBENEA ATAKA WANAOSAMBAZA MAWASILIANO YA SIMU YA NAPE, MAKAMBA, KINANA WACHUKULIWE HATUA

  Malunde       Tuesday, July 23, 2019

Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea ameitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano nchini (TCRA) kutoa taarifa za waliohusika kudukua mawasiliano ya simu ya mbunge wa Mtama, Nape Nnauye na watu wengine.
Wiki iliyopita sauti fupi za mazungumzo ya simu yanayomhusisha Nape, aliyekuwa Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba na makatibu wakuu wastaafu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba zimesambaa kwenye mitandao ya kijamiiAkizungumza na vyombo vya habari  jana  Julai 22, Kubenea alisema kitendo kilichofanyika ni kinyume cha katiba na sheria za nchi ambazo zinatoa uhuru wa faragha kwa mtu.


“Hii ni hatari sana kama viongozi wanafanywa hivi kwa mambo ya faragha kutolewa si hata baadaye watu wanaweza kuvunja ndoa za watu, kama Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amezungumza na hawara kwa mfano ikatoka nje si jambo la hatari hili, kuna vitu ambavyo vinatakiwa kuwa na usiri kwa maana kama hawa ni viongozi tu je wananchi wa kawaida inakuaje..?"Haya mambo hayawezi kufanyika katika nchi inayojali utu wa mtu. TCRA itoe taarifa, ni nani aliyefanya kazi hiyo chafu." AlisemaUsikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post