KOREA KASKAZINI YAFYATUA MAKOMBORA MAWILI | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, July 25, 2019

KOREA KASKAZINI YAFYATUA MAKOMBORA MAWILI

  Malunde       Thursday, July 25, 2019
Korea Kaskazini imerusha kombora la masafa mafupi baharini kulingana na mkuu wa wafanyikazi wa umma nchini Korea Kusini.Makombora hayo yalizinduliwa mapema siku ya Alhamisi , yakisafiri umbali wa kilomita 430 na kupaa angani umbali wa kilomita 50 kabla ya kuanguka katika bahari ya Japan , ambayo pia inajulikana kama bahari ya mashariki.

Hatua hiyo inajiri baada ya taifa hilo kukasirishwa na mipango ya zoezi la pamoja la kijeshi kati ya Marekeni na Korea Kusini linalotarajiwa kufanyika mwezi ujao.

Korea Kaskazini imeonya kwamba mazoezi hayo yatarudisha nyuma mazungumzo ya taifa hilo kutojihami na silaha za kinyuklia.

Kombora la kwanza lilirushwa mwendo wa saa 05.34 mapema alfajiri na la pili mwendo wa 5.57 kulingana na Korea Kusini.

Makombora hayo yalirushwa karibu na mji wa Wonsan. Haijulikani iwapo kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong un alisimamisha uzinduzi huo.

Mtaalam wa silaha nchini Korea Kaskazini Jeffrey Lewis alisema katika ujumbe wake wa twitter kwamba silaha hizo zilifanana kama zile za makombora ya KN-23s.

Kulingana na Lewis wa Taasisi ya masomo ya kimataifa ya Middlebury , makombora ya Kn-23s yanaweza kubeba kichwa cha kombora la nyuklia na kuruka umbali wa kuweza kulenga vikosi vya Marekani nchini Korea Kusini.

Wizara ya ulinzi nchini Korea Kusini imeambia Pyonyang kusitisha vitendo ambavyo ilisema havisaidii kupunguza hali ya wasiwasi , kulingana na chombo cha habari cha reuters.

Waziri wa ulinzi nchini Japan alisema kuwa kombora hilo halikufika katika maji ya Japan na halikuwa na madhara yoyote kwa usalama wa taifa hilo.

Baada ya kumualika kupitia mtandao wa twitter mnamo mwezi Juni, rais Trump na mwenzake wa Korea Kaskazini walifanya kikao katika eneo linalolindwa sana ambalo linagawanya Korea zote mbili ambapo walikubaliana kuanza upya mazungumzo ya kutojihami na silaha za nyuklia .

Baada ya kikao hicho waziri wa ulinzi nchini Marekani Mike Pompeo alisema kuwa mikutano ya kufanyia kazi mpango huo itaanza mwezi Julai lakini kufikia sasa hakujakua na mikutano yoyote kati ya Marekani na maafisa wa Korea kaskazini.

Lakini Korea Kaskazini imeshutumu mpango wa zoezi la kijeshi la pamoja kati ya Marekani na Korea Kusini mwezi ujao , ikiutaja kuwa ukiukaji wa taarifa ya pamoja iliotiwa saini na rais Trump na bwana Kim katika mazungumzo hayo ya ana kwa ana nchini Singapore mwaka uliopita.

''Korea Kaskazini imekasirishwa kwamba Marekani inafanya zoezi la kijeshi la pamoja na Korea Kusini'', alisema Harry Kazianis wa kituo cha Washington cha Maslahi ya kitaifa ambaye alikuwa akizunguma na reuters.

Mwaka uliopita Bwana Kim alisema kwamba Korea Kaskazini itasitisha majaribio yake ya kinyuklia mbali na majaribio yake ya makombora ya masafa marefu.

Vitendo vya Kinyuklia vinaonekana kuendelea na picha za Setlaiti katika kituo kikubwa cha Korea Kaskazini zilionyesha vitendo fulani , madai ambayo huenda taifa hilo likawa na mpango wa kukusanya vifaa vya kutengeza mafuta ya bomu.

Pyongyang pia inaendelea kuonyesha uwezo wake wa kutengeza silaha mpya licha ya vikwazo vyenye masharti makali.

Mapema wiki hii bwana Kim aliikagua manowari yenye muundo mpya , viliripoti vyombo vya habari vya taifa hilo ambayo inaweza kuimarishwa kubeba kombora la masafa marefu kulingana na wachanganuzi.

Pyongayang pia ilifanya jaribio kama hilo la silaha ya masafa mafupi manmo mwezi Mei.

Ni jaribio lake la kwanza kama hilo tangu ifanyie majaribio kombora lake la masafa marefu mwaka 2017.

Bwana Trump alijibu wakati huo kwa kusema anaamini kwamba Kim hawezi kufanya kitu kinachoweza kuathiri mpango wa kuafikia maaamuzi ya uhusiano mwema.

Alituma ujumbe wa twitter kwamba bwana Kim anajua kwamba niko naye na kwamba hataki kuvunja ahadi yake.

-BBC


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post