AFARIKI KWA KUFUKIWA NA KIFUSI AKICHIMBA UDONGO AJENGEE NYUMBA SHINYANGA | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, July 27, 2019

AFARIKI KWA KUFUKIWA NA KIFUSI AKICHIMBA UDONGO AJENGEE NYUMBA SHINYANGA

  Malunde       Saturday, July 27, 2019
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao

Kijana aliyejulikana kwa jina laHassan Tungu (26) amefariki dunia baada ya kuangukiwa na kifusi wakati akichimba kifusi kwa ajili ya matumizi ya kujengea nyumba katika Kitongoji cha Ngaka, Kijiji cha Nyambui, Kata ya Tinde Wilaya ya Shinyanga.


Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao tukio hilo limetokea jana Ijumaa Julai 26,2019 majira ya saa tano na dakika 40 asubuhi.

"Hassan Tungu aliangukiwa na kifusi wakati akichimba kifusi kwa ajili ya matumizi ya kujengea kisha kufa papo hapo. Baada ya kifusi hicho kuanguka pia kiliwajeruhi watu wawili ambao ni Mihambo Mjiga (20) na  Elias Magwala (26)  wote wakazi wa Tinde  na wanapatiwa matibabu katika Kituo cha Afya cha Tinde",amesema Kamanda Abwao.
Na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post