RAIS MAGUFULI AWALILIA WAFANYAKAZI WATANO WA AZAM TV,MADEREVA WALIOFARIKI KWENYE AJALI LEO



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mwenyekiti wa kampuni za Said Salim Bakhresa kufuatia vifo vya wafanyakazi watano wa Azam Media waliopoteza maisha katika ajali ya gari iliyotokea leo tarehe 08 Julai, 2019 eneo la Kizonzo.

"Nimeshtushwa sana na vifo hivi,nampa pole Mwenyekiti ndugu Said Salim Bakhresa,ndugu wa marehemu wote,Mtendaji Mkuu,ndugu Tido Mhando na wafanyakazi wote wa Azam Media Ltd,waandishi wa habari wote na watu wote walioguswa na vifo hivi",- Rais Magufuli.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527