Breaking : WAFANYAKAZI WA AZAM TV WAFARIKI KWENYE AJALI SINGIDA....MAJINA HAYA HAPA


Watu saba wakiwemo wafanyakazi watano wa kampuni ya Azam Media wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori leo asubuhi Jumatatu Julai 8,2019 katika eneo la Shelui wilayani Iramba mkoani Singida.

Inaelezwa kuwa walikuwa wakieleleka wilayani Chato Mkoa wa Geita katika uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Chato-Burigi unaofanyika kesho Jumanne Julai 9, 2019 na Rais wa Tanzania, John Magufuli.

Taarifa kutoka katika kampuni hiyo zinaeleza kuwa wafanyakazi hao walikuwa katika gari aina ya Coaster na kwamba madereva wawili wa magari hayo nao wamefariki dunia.

Waliofariki dunia watano ni wafanyakazi wa Azam TV na madereva wawili wa gari ya kukodi ambao majina yao bado hayajafahamika.

Wafanyakazi wa Azam Tv waliofariki dunia ni: 
Said Haji - Camera man
Charles Wandwi -Camera man
Salim Mhando - Switcher 
Florance Ndibalema- Sound
Sylvanus Kasongo - Engineer 

Majeruhi
Mohamed Mwinshehe 
Mohamed Mainde
Artus Massawe 

Mganga mfawidhi wa hospitali ya Igunga Merichad Magongo amethibitisha kupokea majeruhi watatu katika hospitali ya Igunga.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post