IRAN YAMUITA BALOZI WA UINGEREZA KUHUSIANA NA KUAKAMATWA MELI YAKE | MALUNDE 1 BLOG

Friday, July 5, 2019

IRAN YAMUITA BALOZI WA UINGEREZA KUHUSIANA NA KUAKAMATWA MELI YAKE

  Malunde       Friday, July 5, 2019
Iran imemuita balozi wa Uingereza mjini Tehran kuhusiana na kile ilichosema ni kukamatwa leo kinyume cha sheria meli ya mafuta ya Iran katika kisiwa cha Gibraltar. 

Televisheni ya serikali ya Iran imemnukuu msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Kigeni Abbas Mousavi akithibitisha habari hizo. 

Jeshi la wanamaji wa Uingereza lilikamata meli hiyo ya mafuta ikituhumiwa kwa kupeleka mafuta nchini Syria ikiwa ni hatua ya kukiuka vikwazo vya Umoja wa Ulaya. 

Kitendo hicho kinazusha hofu ya kuongeza mgogoro kati ya nchi za Magharibi na Iran. 

Waziri Kiongozi wa Gibraltar Fabian Picardo alisema katika taarifa kuwa wanaizuilia meli hiyo na shehena yake. 

Meli hiyo inasafiri kwa bendera ya Panama na inaaminika kuwa imebeba mafuta ya Iran.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post