MSANII JAGUAR : 'NIMEKUJA KUTEMBEA TANZANIA NAIPENDA TANZANIA' | MALUNDE 1 BLOG

Friday, July 19, 2019

MSANII JAGUAR : 'NIMEKUJA KUTEMBEA TANZANIA NAIPENDA TANZANIA'

  Malunde       Friday, July 19, 2019Mbunge wa Starehe nchini Kenya, Charles Njagua maarufu Jaguar yupo nchini kuanzia jana. Huku akieleza kuwa atakuwa Tanzania hadi Jumapili Julai 21, 2019.

Akizungumza na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) jana Julai 18, 2019, Jaguar amesema amekuja Tanzania kwa kuwa hana tatizo na Watanzania na kauli aliyoitoa hakuwa amewalenga wao, bali wanaofanya biashara kinyume na taratibu za Kenya.

“Nimekuja kutembea Tanzania naipenda Tanzania na kama unavyojua ile kauli ambayo watu walishindwa kuielewa, nilikuwa namaanisha wanaofanya kazi kinyume na taratibu,” amesisitiza.

Msanii huyo wa wimbo wa 'Kigeugeu' amesema kwamba anapanga kukutana na wabunge marafiki zake wa taifa hilo kama vile Profesa J na Sugu pamoja na wasanii tofauti.

Juni 25, 2019 mbunge huyo ambaye pia ni mwanamuziki kupitia mitandao ya kijamii video yake ilisambaa akieleza kuwafukuza wafanyabiashara wa kigeni wakiwemo Watanzania ndani ya masaa 24 kurudi kwao la sivyo watawapiga na kuwarudisha nchini mwao


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post