BABA LEVO AKUTWA NA KESI YA KUJIBU MAHAKAMANI | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, July 27, 2019

BABA LEVO AKUTWA NA KESI YA KUJIBU MAHAKAMANI

  Malunde       Saturday, July 27, 2019

Mahakama ya Mwanzo ya Mwandiga Mkoani Kigoma, imemkuta na kesi ya kujibu Diwani wa Kata ya Mwanga Revocatus Kipando (Baba Levo), baada ya kutuhumiwa kufanya shambulio kwa Askari wa usalama barabarani akiwa kazini July 15, 2019.

Uamuzi huo umekuja baada Hakimu wa Mahakama hiyo Frolence Ikorongo, kusikiliza upande wa mshitaki akiwa na mashahidi wawili ambao ni Mussa Lukomati na Karume Rashidi, ambao walieleza tukio hilo lilitokea July 15, majira ya saa 1 usiku.

Mashahidi wameeleza kuwa Baba Levo alimshambulia askari anayefahamika kwa jina la Msafiri Ponera, akiwa eneo lake la kazi eneo la Kwabela, na inadaiwa mtuhumiwa alilazimisha kupita kwa pikipiki wakati askari huyo akiwa waruhusu watembea kwa miguu, na baada ya hapo Baba Levo aliamua kumshambulia askari huyo.

Hakimu Ikorongo amesema kuwa, “kifungu cha 240 sura ya 16 kanuni ya adhabu chapisho la mwaka 2002, Mahakama imemkuta mshtakiwa Baba Levo na kesi ya kujibu baada ya kujiridhisha na ushahidi wa mshtaki”

Kesi hiyo imeahirishwa hadi July 30, 2019, ambapo kwa sasa mtuhumiwa Baba levo yuko nje kwa dhamana.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post